Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 114


Sehemu ya 114

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Far West, Missouri, 11 Aprili 1838.

1–2, Nafasi za kanisa zilizoshikiliwa na watu ambao siyo waaminifu zitatolewa kwa watu wengine.

1 Amini hivyo ndivyo asemavyo Bwana: Ni hekima kwa mtumishi wangu David W. Patten, kwamba apange mambo yote ya biashara yake haraka kadiri atakavyoweza, na kugawa bidhaa za biashara yake, ili apate kufanya huduma yangu majira yajayo ya kuchipua, akiambatana na wengine, hata kumi na wawili ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe, ili kulishuhudia jina langu na kutangaza habari njema kwa ulimwengu wote.

2 Kwani amini hivyo ndivyo asemavyo Bwana, kwamba kwa vile wapo watu miongoni mwenu walikataao jina langu, wengine awatapandwa bbadala yao na kupokea uaskofu wao. Amina.