Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 92


Sehemu ya 92

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 15 Machi 1833. Ufunuo unamwelekeza Frederick G. Williams, ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa mshauri kwa Joseph Smith, juu ya majukumu yake katika Kampuni ya Ushirika (ona vichwa vya habari vya sehemu ya 78 na 82).

1–2, Bwana hutoa amri juu ya kujiunga na mpango wa ushirika.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, nimetoa kwa mpango wa ushirika, ulioundwa kulingana na amri nilizotoa hapo awali, ufunuo na amri kuhusu mtumishi wangu Frederick G. Williams, kuwa yawapasa kumpokea katika ushirika. Nisemacho kwa mmoja ninasema kwa wote.

2 Na tena, ninakuambia mtumishi wangu Frederick G. Williams, utakuwa mshiriki hai katika ushirika huu; na kadiri utakavyokuwa mwaminifu katika kushika amri zote za zamani nawe utabarikiwa milele. Amina.

Chapisha