Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 123


Sehemu ya 123

Wajibu wa Watakatifu kuhusu watesi wao, kama ulivyoandikwa na Joseph Smith Nabii, wakati akiwa mfungwa gerezani huko Liberty, Missouri. Sehemu hii ni nukuu kutoka kwenye waraka kwa Kanisa wa 20 Machi 1839 (ona kichwa cha habari kwa sehemu ya 121).

1–6, Watakatifu wanapaswa kukusanya na kuchapisha historia ya taabu na mateso yao; 7–10, Roho yule yule aliyeanzisha mafundisho ya imani za uongo pia huongoza kuteswa kwa Watakatifu; 11–17, Wengi miongoni mwa madhehebu yote hatimaye wataupokea ukweli.

1 Na tena, tungelipendekeza ili mpate kufikiria utaratibu wa watakatifu wote kukusanya ukweli wote, juu ya mateso na maonevu yote waliyofanyiwa na watu wa Jimbo hili;

2 Na pia wa mali yote na kiwango cha uharibifu wamefanyiwa, wa sifa na majeraha ya binafsi, vile vile ya mali isiyohamishika;

3 Na pia majina ya watu wote ambao wameshiriki katika unyanyasaji wao, kwa kadiri watakavyoweza kuwapata na kuwagundua.

4 Na pengine kamati yaweza kuteuliwa kuchunguza mambo haya, na kuchukua maelezo na hati za viapo; na pia kukusanya makala za kashfa ambazo zimezagaa;

5 Na yote yaliyomo katika magazeti, na katika ensaiklopidia, na historia zote za kashfa ambazo zimechapishwa, na zinazoandikwa, na ni nani, na kuwakilisha mlolongo mzima wa uhuni wa kiibilisi na uovu na matumizi ya mauaji ambayo yamefanyika kwa watu hawa—

6 Ili tupate si kuchapisha tu kwa walimwengu wote, bali kuzikabidhi kwa viongozi wa serikali katika giza na rangi yao yote ya jehanamu, kama jitihada za mwisho ambazo zimeunganishwa kwetu sisi na Baba yetu wa Mbinguni, kabla hatujaweza kudai kiukamilifu na kwa utimilifu ahadi ile ambayo itamwita yeye kutoka mahali pake pa akujificha; na pia ili taifa lote lipate kuachwa pasipo udhuru kabla yeye hajatuma uwezo wa mkono wake wenye nguvu.

7 Ni kazi muhimu ambayo tunadaiwa na Mungu, na malaika, ambao pamoja nao tutasimamishwa, na pia kwetu sisi wenyewe, kwa wake zetu na watoto, ambao wamefanywa wainame chini kwa huzuni, uchungu, na mashaka, chini ya mkono uliolaaniwa wa uuaji, udhalimu, na ukandamizaji, ukisaidiwa na kuhimizwa na kuungwa mkono na nguvu za yule roho ambaye kwa nguvu sana ameyapiga ribiti mafundisho ya imani ya mababu, ambao wamerithisha uongo, juu ya mioyo ya watoto, na kuujaza ulimwengu kwa machafuko, na amekuwa akikua na kuwa imara na imara, na sasa ndiyo chimbuko kuu la uharibifu wote, na aulimwengu mzima unaugulia chini ya uzito wa uovu wake.

8 Ni anira ya chuma, ni kamba ngumu; wao ndiyo zile pingu za mikono, na minyororo, na vipingamizi, na pingu za miguu za jehanamu.

9 Kwa hiyo ni kazi muhimu tunayodaiwa, siyo tu kwa wake zetu wenyewe na watoto, bali kwa wajane na kwa wasio na baba, ambao waume zao na baba zao awameuawa chini ya mkono wake wa chuma;

10 Ambaye giza na matendo yake meusi yanatosha kuifanya jehanamu yenyewe itetemeke, na kusimama kwa mshangao na woga, na mikono ya ibilisi mwenyewe itetemeke na kupooza.

11 Na pia ni kazi muhimu ambayo tunadaiwa na kizazi chote kinachochipukia, na kwa wote walio safi moyoni—

12 Kwani bado wako wengi duniani miongoni mwa vikundi vyote, vyama, na madhehebu, ambao awanapofushwa na ustadi wa ujanja wa wanadamu, ambao huvizia ili kudanganya, na ambao huzuiliwa kuupata ukweli kwa sababu tu bhawajui mahali pa kuupata—

13 Kwa hiyo, kwamba yatupasa kutumia maisha yetu katika kuyaleta kwenye nuru mambo yote ya giza, ayaliyofichwa; kadiri tunavyoyajua; nayo hakika yanafunuliwa kutoka mbinguni—

14 Haya ndiyo yanapaswa kushughulikiwa kwa bidii zaidi.

15 Acha mtu yeyote asiyahesabu kama ni mambo madogo madogo; kwani kuna mengine yajayo hapo baadaye, kuhusiana na watakatifu, ambao wanayategemea mambo haya.

16 Mnajua, ndugu, kwamba merikebu kubwa ahufaidika kwa kiwango kikubwa sana na usukani mdogo wakati wa dhoruba, kwa kuwekwa katika kutenda kazi dhidi ya upepo na mawimbi.

17 Kwa hiyo, ndugu wapendwa, kwa afuraha na tufanye mambo yote yaliyo katika uwezo wetu; na ndipo tusimame imara, kwa uhakika mkubwa, kuuona bwokovu wa Mungu, na kwa mkono wake kufunuliwa.