Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 74


Sehemu ya 74

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii, Wilaya ya Wayne, New York mwaka 1830. Hata kabla ya kuanzishwa kwa Kanisa, maswali yalikuwa yameibuka juu aina sahihi ya ubatizo, maswali ambayo yalimwongoza Nabii kutafuta majibu juu ya mada hii. Historia ya Joseph Smith inaeleza kwamba ufunuo huu ni maelezo juu ya 1 Wakorintho 7:14, andiko ambalo mara nyingi limekuwa likitumika kuhalalisha ubatizo wa watoto wachanga.

1–5, Paulo alishauri Kanisa la siku zake lisizishikilie torati ya Musa; 6–7, Watoto wadogo ni watakatifu na wametakaswa kwa njia ya Upatanisho.

1 Kwani mume aasiye amini anatakaswa na mke, na mke asiye amini anatakaswa na mume; vinginevyo watoto wenu wangelikuwa wachafu, lakini sasa ni watakatifu.

2 Sasa, katika siku za mitume sheria ya tohara ilikuwepo miongoni mwa Wayahudi wote ambao hawakuamini injili ya Yesu Kristo.

3 Na ikawa kwamba kulitokea augomvi mkubwa miongoni mwa watu kuhusu sheria ya btohara, kwani mume asiye amini alitaka watoto wake watahiriwe na kuwa chini ya ctorati ya Musa, torati ambayo ilikwisha timilizwa.

4 Na ikawa kwamba watoto wale, ambao walilelewa chini ya torati ya Musa, walifuata amapokeo ya Baba zao na hawakuamini injili ya Yesu Kristo, kwa njia hii hawakuwa watakatifu.

5 Kwa hiyo, kwa sababu hii, mtume aliliandikia kanisa, akiwapa amri, siyo ya Bwana, bali yake yeye mwenyewe, kwamba mwenye kuamini hapaswi akuungana na asiye amini; isipokuwa btorati ya Musa imekoma miongoni mwao,

6 Ili watoto wao waweze kubaki bila tohara; na ili mapokeo yaweze kukoma, ambayo husema watoto wadogo siyo watakatifu; kwani imekuwepo miongoni mwa Wayahudi;

7 Lakini awatoto wadogo ni bwatakatifu, wakiwa cwametakaswa kwa njia ya dupatanisho wa Yesu Kristo; na hiki ndicho maandiko yanachomaanisha.