Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 95


Sehemu ya 95

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 1 Juni 1833. Ufunuo huu ni mfululizo wa maelekezo matakatifu ya kujenga nyumba kwa ajili ya kuabudu na mafundisho nyumba ya Bwana (ona sehemu ya 88:119–136).

1–6, Watakatifu wanakemewa kwa kushindwa kwao kujenga nyumba ya Bwana; 7–10, Bwana anataka kuitumia nyumba Yake kwa kuwapa endaomenti watu Wake kwa uwezo utokao juu; 11–17, Nyumba hiyo iwekwe wakfu kama mahali pa kuabudu na kwa ajili ya shule ya Mitume.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwenu ninyi ambao ninawapenda, na wale niwapendao pia ahuwarudi ili dhambi zao ziweze bkusamehewa, kwani pamoja na kuwarudi ninawatayarishia njia kwa ajili ya cukombozi wao katika mambo yote yatokanayo na dmajaribu, na nimewapenda ninyi—

2 Kwa hiyo, ninyi yafaa kuwarudi na kukemewa mbele ya uso wangu;

3 Kwani ninyi mmenitendea dhambi kubwa, kwa sababu hamkuipa umuhimu amri ile iliyo kuu katika mambo yote, ambayo nimeitoa kwenu juu ya ujenzi wa anyumba yangu;

4 Kwa ajili ya matayarisho ambayo ninapanga kuwatayarisha mitume wangu kwa ajili ya akupogoa shamba langu la mizabibu kwa mara ya mwisho, ili nipate kulitimiza tendo langu la bajabu, ili niweze ckumwaga Roho yangu juu ya watu wote—

5 Lakini tazama, amini ninawaambia, kwamba wako wengi waliotawazwa miongoni mwenu, ambao nimewaita lakini ni wachache kati yao awalioteuliwa.

6 Wale ambao hawajateuliwa wametenda dhambi mbaya sana, kwa sababu wanatembea agizani saa sita mchana.

7 Na kwa sababu hii niliwapa ninyi amri ya kwamba yawapasa kuitisha akusanyiko lenu la kiroho, ili bkufunga kwenu na kuomboleza kwenu kuweze kupaa juu masikioni mwa Bwana wa cSabato, ambaye kwa tafsiri, ni dmuumba wa siku ya kwanza, mwanzo na mwisho.

8 Ndiyo, amini ninawaambia, niliwapa amri ya kwamba mjenge nyumba, ambamo ndani ya nyumba hiyo ninapanga kuwapa aendaomenti wale ambao nimewateua kwa uwezo utokao juu;

9 Kwani hii ndiyo aahadi ya Baba kwenu ninyi; kwa hiyo ninawaamuru ninyi kaeni humu, hata kama wale mitume wangu wa Yerusalemu.

10 Hata hivyo, watumishi wangu walitenda dhambi kubwa sana; na aushindani ulianza katika bshule ya manabii; ambao yalikuwa ya kuhuzunisha kwangu, asema Bwana; kwa sababu hiyo, niliwatoa ili kuwarudi.

11 Amini ninawaambia, ni mapenzi yangu kuwa mjenge nyumba. Kama mtazishika amri zangu mtapata uwezo wa kuijenga.

12 Kama ahamtazishika amri zangu, bupendo wa Baba hautakuwamo ndani yenu, kwa hiyo mtatembea gizani.

13 Sasa hapa ndipo ilipo hekima, na mapenzi ya Bwana—nyumba na ijengwe, siyo kwa jinsi ya ulimwengu, kwani siwaruhusu ninyi kuishi kwa jinsi ya ulimwengu;

14 Kwa hiyo, na ijengwe kwa jinsi ambayo nitaionyesha kwa watatu kati yenu, ambao mtawachagua na kuwaweka katika mamlaka haya.

15 Na ukubwa wake utakuwa futi hamsini na tano katika upana, na iwe futi sitini na tano katika urefu, katika ukumbi wake wa ndani.

16 Na sehemu ya chini ya ukumbi wa ndani uwekwe wakfu kwangu kwa ajili ya sakramenti na matoleo, na kwa ajili ya kuhubiri kwenu, na kufunga kwenu, na kuomba kwenu, na kwa akunitolea matakwa yenu yaliyo matakatifu sana, asema Bwana wenu.

17 Na sehemu ya juu ya ukumbi wa ndani iwekwe wakfu kwangu kwa ajili ya shule ya mitume wangu, asema Mwana aAmani; au, kwa maneno mengine, Alfa, au, kwa maneno mengine, Omega; hata Yesu Kristo bBwana wenu. Amina.