Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 65


Sehemu ya 65

Ufunuo juu ya sala uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Hiram, Ohio, 30 Oktoba 1831.

1–2, Funguo za ufalme wa Mungu zakabidhiwa kwa mwanadamu duniani, na kazi ya injili itashinda; 3–6, Ufalme wa mbinguni wa milenia utakuja na kuungana na ufalme wa Mungu wa duniani.

1 Sikilizeni, na lo, sauti ya mtu kama aliyetumwa kutoka juu, mwenye uwezo na mwenye nguvu, ambaye kutoka kwake ni hata mwisho wa dunia, ndiyo, ambaye sauti yake yaenda kwa wanadamu—aItengenezeni njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.

2 aFunguo za bufalme wa Mungu zakabidhiwa kwa mwanadamu duniani, na kutoka huko injili itaenea hata miisho ya dunia, kama vile cjiwe lililochongwa mlimani bila kazi ya mikono litabiringika, hadi dlitaijaza dunia yote.

3 Ndiyo, sauti iliayo—Itengenezeni njia ya Bwana, andaeni akaramu ya Mwanakondoo, kuweni tayari kwa ajili ya bBwana Harusi.

4 Ombeni kwa Bwana, mlilingane jina lake takatifu, wajulisheni watu matendo yake ya ajabu.

5 Mlinganeni Bwana, ili ufalme wake uweze kuenea juu ya dunia, ili wakazi wake waweze kuupokea, na kujitayarisha kwa ajili ya siku zijazo, siku ambazo Mwana wa Mtu aatashuka kutoka mbinguni, baliyevikwa katika mngʼaro wa cutukufu wake, kukutana na dufalme wa Mungu ambao umewekwa duniani.

6 Kwa hiyo, na aufalme wa Mungu uenee, ili bufalme wa mbinguni uweze kuja, ili wewe, Ee Mungu uweze kutukuzwa mbinguni hata na duniani, ili adui zako waweze kushindwa; kwa kuwa ukuu ni cwako, uwezo na utukufu, milele na milele. Amina.