Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 129


Sehemu ya 129

Mafundisho yaliyotolewa na Joseph Smith Nabii, huko Nauvoo, Illinois, 9 Februari 1843, ambayo yanaelezea funguo kuu tatu ambazo kwa hizo twaweza kutofautisha aina sahihi za malaika na roho wahudumu.

1–3, Mbinguni kuna miili ya waliofufuka na miili ya kiroho; 4–9, Funguo zimetolewa ambazo kwa hizo wajumbe kutoka ngʼambo ya pazia wanaweza kutambulika.

1 Kuna viumbe wa aina mbili ambinguni, nao ni: bMalaika, ambao ni watu cwaliofufuka, wenye miili ya nyama na mifupa—

2 Kwa mfano, Yesu alisema: Nishikenishikeni na mwone, kwa kuwa roho haina amwili na mifupa, kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.

3 Ya pili, ni aroho za watu wenye bhaki waliokamilika, wale ambao hawajafufuka, lakini wanarithi utukufu huo huo

4 Wakati mjumbe akija akisema anao ujumbe kutoka kwa Mungu, mpe mkono wako na mwombe mshikane mikono.

5 Kama yeye atakuwa malaika atafanya hivyo, nawe utausikia mkono wake.

6 Kama atakuwa roho ya mtu mwenye haki aliyekamilika yeye atakuja katika utukufu wake; kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee anayoweza kuonekana—

7 Mwombe mshikane mikono, lakini yeye hatafanya lolote, kwa sababu ni kinyume cha utaratibu wa mbinguni kwa mtu mwenye haki kudanganya; lakini yeye bado atatoa ujumbe wake—

8 Lakini ikiwa ni ya aibilisi akiwa kama malaika wa nuru, ukimwomba kushikana mikono naye atakupa mkono wake, na wewe hutasikia chochote; nawe utaweza kumgundua.

9 Hizi ndizo funguo kuu tatu ambazo kwa njia hiyo ninyi mtaweza kujua iwapo huduma yoyote yatoka kwa Mungu.