Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 103


Sehemu ya 103

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 24 Februari 1834. Ufunuo huu ulipokelewa baada ya kuwasili huko Kirtland, Ohio, kwa Parley P. Pratt na Lyman Wight, ambao walikuja kutoka Missouri ili kushauriana na Nabii juu ya kuwapelekea msaada na urejesho wa Watakatifu kwenye ardhi yao katika Wilaya ya Jackson.

1–4, Kwa nini Bwana aliruhusu Watakatifu katika Wilaya ya Jackson kuteswa; 5–10, Watakatifu watashinda ikiwa watashika amri; 11–20, Ukombozi wa Sayuni utakuja kwa uwezo, na Bwana atakwenda mbele ya watu Wake; 21–28, Watakatifu watakusanyika katika Sayuni, na wale ambao huutoa uhai wao watauona tena; 29–40, Ndugu kadhaa wanaitwa kuunda Kambi ya Sayuni na kwenda Sayuni; wanaahidiwa ushindi ikiwa watakuwa waaminifu.

1 Amini ninawaambia, marafiki zangu, tazama, nitawapa ufunuo na amri, ili mpate kujua namna ya akutenda katika kutimiza majukumu yenu juu ya wokovu na bukombozi wa ndugu zenu, ambao wametawanywa juu ya nchi ya Sayuni;

2 Wakiwa awamefukuzwa na kupigwa kwa mikono ya adui zangu, ambao nitawamwagia ghadabu pasipo kipimo katika wakati wangu.

3 Kwani nimewavumilia vya kutosha, ili wapate akujaza kipimo cha uovu wao, ili kikombe chao kipate kujaa;

4 Na ili wale wajiitao wenyewe kwa jina langu wapate akurudiwa kwa kipindi kifupi kwa adhabu iliyo kali na chungu, kwa sababu bhawakutii kabisa mausia na amri ambazo niliwapa.

5 Lakini amini ninawaambia, kwamba nimeagiza agizo ambalo watu wangu watalipata, ilimradi tu watu wangu watatii kutoka saa hii aushauri ambao Mimi, Bwana Mungu wao, nitautoa kwao.

6 Tazama watashinda, kwani nimeagiza, waanze kushinda dhidi ya adui zangu kutoka saa hii.

7 Na kuwa awaangalifu kwa maneno yote ambayo Mimi, Bwana Mungu wao, nitasema kwao, kamwe hawatakoma kushinda hadi bfalme za ulimwengu ziwekwe chini ya miguu yangu, na dunia citolewe kwa dwatakatifu, ili ekuimiliki milele na milele.

8 Lakini kadiri awasivyozishika amri zangu, na wala hawaangalii kutii maneno yangu yote, falme za ulimwengu zitawashinda.

9 Kwani wao waliwekwa kuwa anuru kwa ulimwengu, na kuwa njia ya wokovu kwa wanadamu;

10 Na ilimradi wao sio njia ya wokovu kwa wanadamu, wao ni sawa sawa na achumvi iliyopoteza ladha yake, na haifai tena kwa lolote ila kutupwa nje na kukanyagwa chini ya miguu ya watu.

11 Lakini amini ninawaambia, nimeazimia kwamba ndugu zenu ambao wametawanywa watarudi katika anchi ya urithi wao, na kujenga mahali palipoharibiwa pa Sayuni.

12 Kwa kuwa baada ya ataabu nyingi, kama nilivyosema kwenu katika amri ya zamani, huja baraka.

13 Tazama, hii ndiyo baraka niliyoahidi baada ya masumbuko yenu, na masumbuko ya ndugu zenu—ukombozi wenu, na ukombozi wa ndugu zenu, hata urejesho wao katika nchi ya Sayuni, ili kuwaimarisha, kamwe wasitupwe chini tena.

14 Hata hivyo, endapo watauchafua urithi wao watatupwa chini; kwani sitawahurumia kama watachafua urithi wao.

15 Tazama, ninawaambia, ukombozi wa Sayuni hauna budi kuja kwa uwezo;

16 Kwa hiyo, nitawainulia watu wangu mtu, ambaye atawaongoza kama jinsi aMusa alivyowaongoza wana wa Israeli.

17 Kwani ninyi ni wana wa Israeli, na wa auzao wa Ibrahimu, na ninyi hamna budi kuongozwa kutoka utumwani kwa uwezo, na kwa mkono ulionyoshwa.

18 Na kama vile baba zenu walivyoongozwa zamani, hivyo ndivyo ukombozi wa Sayuni utakavyokuwa.

19 Kwa hiyo, msiache mioyo yenu ikate tamaa, kwani siwaambii ninyi kama nilivyowaambia baba zenu: aMalaika wangu atatangulia mbele yenu, lakini sio buwepo wangu.

20 Lakini ninawaambia: Kuwa amalaika wangu watatangulia mbele yenu, na pia uwepo wangu, na hatimaye bmtaimiliki nchi iliyo bora.

21 Amini, amini ninawaambia, kwamba mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, ndiye amtu ambaye nilimfananisha na mtumishi ambaye Bwana wa bshamba alimzungumzia katika mfano ambao nimewapa.

22 Kwa hiyo acheni mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, aseme na anguvu ya nyumba yangu, vijana wangu wa kiume na walio na umri wa kati—Jikusanyeni pamoja katika nchi ya Sayuni, juu ya nchi ambayo nimeinunua kwa fedha ambayo imewekwa wakfu kwa ajili yangu.

23 Na makanisa yote yawatume watu wao wenye hekima pamoja na fedha, na awanunue ardhi kama nilivyowaamuru.

24 Na kadiri maadui zangu wanavyokuja dhidi yenu ili kuwafukuza kutoka katika aardhi yangu iliyo bora, ambayo nimeiweka wakfu kuwa nchi ya Sayuni, hata nchi yenu wenyewe baada ya shuhuda hizi, ambazo mmeniletea mbele yangu dhidi yao, ninyi mtawalaani.

25 Na yeyote mtakayemlaani, nitamlaani, nanyi mtanipatia haki na adui zangu.

26 Na uwepo wangu utakuwepo kati yenu hata katika akunipatia haki mimi na adui zangu, hata kwa kizazi cha tatu na cha nne cha wale wanichukiao Mimi.

27 Na mtu yeyote asiogope akuutoa uhai wake kwa ajili yangu; kwa kuwa yeyote autoaye uhai wake kwa ajili yangu atauona tena.

28 Na yeyote asiye kuwa tayari kuutoa uhai wake kwa ajili yangu siyo mwanafunzi wangu.

29 Ni mapenzi yangu kuwa mtumishi wangu aSidney Rigdon akainue sauti yake katika mikutano katika nchi za mashariki, katika kuyatayarisha makanisa kushika amri ambazo nimewapa juu ya urejesho na ukombozi wa Sayuni.

30 Ni mapenzi yangu kwamba mtumishi wangu aParley P. Pratt na mtumishi wangu Lyman Wight wasirudi katika nchi ya ndugu zao, hadi wao watakapokuwa wamepata watu wa kuongozana nao kwenda nchi ya Sayuni, kwa makumi, au kwa ishirini, au kwa hamsini, au kwa mamia, hadi watakapokuwa wamepata idadi ya mia tano ya bnguvu ya nyumba yangu.

31 Tazama haya ndiyo mapenzi yangu; ombeni nanyi mtapata; lakini wanadamu asiyo mara kwa mara hufanya mapenzi yangu.

32 Kwa hiyo, kama hamwezi kuwapata mia tano, tafuteni kwa bidii kwamba pengine mtaweza kuwapata mia tatu.

33 Na kama hamwezi kuwapata mia tatu, tafuteni kwa bidii kwamba pengine mtaweza kuwapata mia moja.

34 Lakini amini ninawaambia, amri ninawapa, ya kwamba msiende katika nchi ya Sayuni hadi ninyi mmewapata watu mia wa nguvu ya nyumba yangu, ili kwenda pamoja nanyi katika nchi ya Sayuni.

35 Kwa hiyo, kama nilivyowaambia, ombeni nanyi mtapewa; ombeni kwa dhati ili pengine mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, apate kwenda pamoja nanyi, na kuongoza katikati ya watu wangu, na kuanzisha ufalme wangu juu ya nchi iliyowekwa awakfu, na kuwaimarisha watoto wa Sayuni juu ya sheria na amri ambazo zilikuwepo na ambazo zitatolewa kwenu.

36 Vyote, ushindi na utukufu vitapatikana kwenu kutokana na abidii yenu, uaminifu, na bsala za imani.

37 Na mtumishi wangu Parley P. Pratt asafiri pamoja na mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo.

38 Na mtumishi wangu Lyman Wight asafiri pamoja na mtumishi wangu Sidney Rigdon.

39 Na mtumishi wangu Hyrum Smith asafiri pamoja na mtumishi wangu Frederick G. Williams.

40 Na mtumishi wangu Orson Hyde asafiri pamoja na mtumishi wangu Orson Pratt, kokote ambako mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, atakakowashauri, katika kupata ukamilifu wa amri hizi ambazo nimewapa, na mengine yote yaacheni mikononi mwangu. Hivyo ndivyo. Amina.