Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 66


Sehemu ya 66

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Hiram, Ohio, 29 Oktoba 1831. William E. McLellin alimwomba Bwana kwa siri kumjulisha kupitia kwa Nabii jibu kwa maswali matano, ambayo hayakuwa yamejulikana kwa Joseph Smith. Kwa ombi la McLellin Nabii alimwuliza Bwana na akapokea ufunuo huu.

1–4, Agano lisilo na mwisho ndiyo utimilifu wa injili; 5–8, Wazee wafundishe, washuhudie, na kusemezana na watu; 9–13, Huduma ya utumishi wa uaminifu humhakikishia urithi wa uzima wa milele.

1 Tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwa mtumishi wangu William E. McLellin—Heri wewe, kwa kuwa umegeuka na kuacha uovu wako, na umepokea ukweli wangu, asema Bwana Mkombozi wako, Mwokozi wa ulimwengu, hata wengi kama awataliamini jina langu.

2 Amini ninakuambia, heri wewe kwa kuwa umepokea aagano langu lisilo na mwisho, hata utimilifu wa injili yangu, iliyotolewa kwa wanadamu, ili wawe na buzima na kufanywa kuwa washiriki wa utukufu ambao utafunuliwa katika siku za mwisho, kama vile ilivyoandikwa na manabii na mitume katika siku za kale.

3 Amini ninakuambia, mtumishi wangu William, kwamba wewe u safi, lakini siyo kabisa; tubu mambo yale ambayo hayapendezi machoni mwangu, asema Bwana, kwani Bwana aatayaonyesha kwako.

4 Na sasa, amini, Mimi, Bwana, nitakuonyesha mapenzi yangu juu yako, au mapenzi yangu ni nini juu yako.

5 Tazama, amini ninakuambia, kuwa ni mapenzi yangu kuwa autangaze injili yangu kutoka nchi hadi nchi, na kutoka mji hadi mji, ndiyo, katika maeneo ya karibu mahali ambako haijatangazwa.

6 Usikae siku nyingi mahali hapa; bado usiende kwenye nchi ya Sayuni; lakini kadiri unavyoweza kutuma, tuma; vinginevyo usiifikirie mali yako.

7 aNenda nchi za mashariki, toa bushuhuda kila mahali, kwa watu wote na katika masinagogi yao, na ukisemezana na watu.

8 Na mtumishi wangu Samuel H. Smith aende pamoja na wewe, na wala usimwache, na umpe maelekezo; na yule aliye mwaminifu atafanywa kuwa aimara kila mahali; na Mimi, Bwana, nitakwenda pamoja nawe.

9 Weka amikono yako juu ya wagonjwa, nao bwatapona. Usirudi hadi Mimi, Bwana, nitakapokutuma. Uwe mvumilivu katika mateso. cOmba nawe utapata; bisha, nawe utafunguliwa.

10 Usitafute kujihangaisha. Acha uovu wote. aUsizini—jaribu ambalo limekuwa likikutatiza.

11 aShika maneno haya, kwani ni ya kweli na kuaminika; nawe uitukuze huduma iliyo yako, na wasukume watu wengi kwenda bSayuni cwakiimba na shangwe isiyo na mwisho itakuwa juu ya vichwa vyao.

12 aUendelee katika mambo haya hata mwisho, nawe utapata btaji la uzima wa milele katika mkono wa kuume wa Baba yangu, ambaye amejaa neema na ukweli.

13 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana aMungu wako, Mkombozi wako, hata Yesu Kristo. Amina.