Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 86


Sehemu ya 86

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 6 Desemba 1832. Ufunuo huu ulipokelewa wakati Nabii alipokuwa akihakiki na kuhariri muswada wa tafsiri ya Biblia.

1–7, Bwana anatoa maana ya mfano wa ngano na magugu; 8–11, Anaelezea baraka za ukuhani kwa wale ambao ni warithi kisheria kwa jinsi ya mwili.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwenu ninyi watumishi wangu, kuhusu amfano wa ngano na magugu:

2 Tazama, amini ninasema, lile konde ni ulimwengu, na mitume walikuwa ni wapanda mbegu;

3 Na baada ya kuwa wamelala mtesaji mkuu wa kanisa, muasi, kahaba, hata aBabilonia, yule ayafanyaye mataifa yote kunywa kikombe chake, ambao katika mioyo yao adui, hata Shetani, hukaa na kutawala—tazama yeye ndiye hupanda magugu; kwa hiyo, magugu huikaba ngano na kulifukuzia bkanisa nyikani.

4 Lakini tazama, katika asiku za mwisho, hata sasa wakati Bwana anapoanza kulileta neno, na jani linapoanza kumea na likiwa bado changa—

5 Tazama, amini ninawaambia, amalaika wanamlilia Bwana usiku na mchana, ambao wako tayari na wanasubiri kutumwa ili bkuyakata chini makonde;

6 Lakini Bwana huwaambia, msiyangʼoe magugu wakati jani likiwa bado changa (kwani amini imani yenu ni dhaifu), msije mkaharibu na ngano pia.

7 Kwa hiyo, acha ngano na magugu yakue pamoja hadi mavuno yatakapokuwa yameiva kikamilifu; ndipo kwanza mtaikusanya ngano kutoka miongoni mwa magugu, na baada ya kuikusanya ngano, tazama na lo, magugu yamefungwa matita matita, na konde limebaki kwa kuchomwa.

8 Kwa hiyo, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwenu ninyi, ambao aukuhani umedumu kupitia safu ya uzao wa baba zenu—

9 Kwani ninyi ni awarithi kisheria, kwa jinsi ya mwili, na bmkafichwa kutoka ulimwenguni, pamoja na Kristo katika Mungu—

10 Kwa hiyo maisha yenu na ukuhani vimedumu, na havina budi kudumu kupitia ninyi na safu ya uzao wenu hata zije zama za aurejesho wa vitu vyote vilivyonenwa kwa vinywa vya manabii wote watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.

11 Kwa hiyo, heri ninyi kama mtakaa katika wema wangu, na anuru ya kuwa mwangaza kwa Wayunani, na kupitia ukuhani huu, mwokozi kwa watu wangu, bIsraeli. Bwana amesema hili. Amina.