Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 47


Sehemu ya 47

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith, Nabii, huko Kirtland, Ohio, 8 Machi 1831. John Whitmer, ambaye alikuwa tayari ametumika kama karani kwa Nabii, mwanzoni alisita wakati alipoombwa kutumikia kama mwanahistoria na mtunza kumbukumbu wa Kanisa, akiwa akichukua nafasi ya Oliver Cowdery. Aliandika, “Nisingelitaka kufanya hili lakini natamani kuona mapenzi ya Bwana yatimie, na kama ndivyo anavyotaka, natamani kwamba angenionyesha kupitia kwa Joseph Mwonaji.” Baada ya Joseph Smith kupokea ufunuo huu, John Whitmer alikubali na kutumikia katika ofisi aliyoteuliwa.

1–4, John Whitmer ateuliwa kutunza historia ya Kanisa na kuwa mwandishi wa Nabii.

1 Tazama, ni muhimu kwangu kwamba mtumishi wangu John aandike na atunze ahistoria ya kila siku, na akusaidie wewe, Joseph mtumishi wangu, katika kuandika mambo yote utakayopewa, hadi atakapoitwa kwa kazi nyingine,

2 Tena, amini ninakuambia kuwa aweza kupaza sauti yake katika mikutano, popote itakapofanyika.

3 Na tena, ninawaambia kuwa atateuliwa kuandika kumbukumbu na historia ya kanisa daima; kwani Oliver Cowdery nimemteua katika ofisi nyingine.

4 Kwa hiyo, itatolewa kwake na aMfariji, kuandika mambo haya kadiri yeye atakavyokuwa mwaminifu. Hivyo ndivyo. Amina.