Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 54


Sehemu ya 54

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, kwa Newel Knight, huko Kirtland, Ohio, 10 Juni 1831. Waumini wa Kanisa wanaoishi huko Thompson, Ohio, waligawanyika juu ya maswali yahusianayo na kuwekwa wakfu kwa mali. Uchoyo na uroho vilijitokeza. Kufuatia misheni yake kwa Shakers (ona kichwa cha habari cha sehemu ya 49). Leman Copley alivunja agano lake la kuweka wakfu shamba lake kubwa kama mahali pa urithi, kwa Watakatifu waliowasili kutoka Colesville, New York. Kama matokeo, Newel Knight (kiongozi wa waumini walioishi katika Thompson) na wazee wengine walikuwa wamekuja kwa Nabii wakiomba mwongozo namna ya kuendelea. Nabii alimwomba Bwana na akapokea ufunuo huu, ambao unawaamuru waumini katika Thompson kuliacha shamba la Leman Copley na kusafiri kwenda Missouri.

1–6, Watakatifu lazima washike agano la injili ili kupata rehema; 7–10, Lazima wawe na subira katika taabu.

1 Tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, hata aAlfa na Omega, mwanzo na mwisho, hata yule baliyesulubiwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu—

2 Tazama, amini, amini, ninakuambia, mtumishi wangu Newel Knight, simama imara katika ofisi niliyokuteua.

3 Na kama ndugu zako wanataka kuwakwepa adui zao, na watubu dhambi zao zote, na kuwa awanyenyekevu na kweli na wanyoofu mbele zangu.

4 Na kwa kuwa aagano ambalo walifanya kwangu limevunjwa, na hata hivyo limekuwa bure na blimebatilika.

5 Na ole wake mtu aliletaye jambo la akukosesha, kwani ingekuwa heri kwake kama angetoswa katika kilindi cha bahari.

6 Lakini wana heri wale ambao wameshika agano na kufuata amri, kwani watapata arehema.

7 Kwa hiyo, enendeni sasa na muikimbie nchi hii, wasije adui zenu wakaja juu yenu; na anzeni safari yenu, na mchagueni yule mumtakaye kuwa kiongozi wenu, na kulipa fedha kwa ajili yenu.

8 Na hivyo mtafanya safari yenu katika mikoa ya magharibi, kwenye nchi ya aMissouri, kwenye mipaka ya Walamani.

9 Na baada ya kufanya safari, tazama, ninawaambia, tafuteni amaisha kama watu wengine, hadi nitakapotayarisha mahali kwa ajili yenu.

10 Na tena, kuweni awavumilivu katika taabu hadi bnijapo; na tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, na wale ambao cwamenitafuta mapema watapata dpumziko nafsini mwao. Hivyo ndivyo. Amina.