Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 3


Sehemu ya 3

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii, huko Harmony, Pennsylvania, Julai 1828, kuhusiana na upotevu wa kurasa 116 za muswada ulio tafsiriwa kutoka sehemu ya kwanza ya Kitabu cha Mormoni, ambacho kiliitwa kitabu cha Lehi. Nabii huku akisita aliruhusu kurasa hizi kutoka mikononi mwake na kwenda katika mikono ya Martin Harris, ambaye alitumika kwa kipindi kifupi kama mwandishi katika tafsiri ya Kitabu cha Mormoni. Ufunuo huu ulitolewa kupitia Urimu na Thumimu. (Ona sehemu ya 10.)

1–4, Mwelekeo wa Bwana ni imara milele; 5–15, Joseph Smith lazima atubu au atapoteza kipawa cha kutafsiri; 16–20, Kitabu cha Mormoni kimekuja kwa ajili ya kuokoa uzao wa Lehi.

1 aKazi, na mipango, na malengo ya Mungu hayawezi kubatilishwa, wala hayawezi kuwa kazi bure.

2 Kwani aMungu haenendi katika njia zisizo nyoofu, wala hageuki mkono wa kulia wala wa kushoto, wala habadilishi kauli kutoka ile aliyosema, hivyo njia zake ni nyoofu, na bmwelekeo wake ni imara milele.

3 Kumbuka, kumbuka kwamba siyo akazi ya Mungu ambayo hubatilika, bali ni kazi ya wanadamu;

4 Kwani ingawa mwanadamu aweza kupata mafunuo mengi, na kuwa na uwezo wa kufanya matendo mengi na makubwa, lakini kama aatajivuna katika nguvu zake, na kupuuza bushauri wa Mungu, na kufuata mwongozo wa matakwa yake mwenyewe na tamaa za ckimwili, lazima ataanguka, na kujiletea mwenyewe dkisasi cha Mungu wa haki juu yake.

5 Tazama, umeaminiwa juu ya mambo haya, lakini ni kali namna gani amri zako; na kumbuka pia ahadi ambazo zimewekwa kwako, kama hungezivunja.

6 Na tazama, ni mara ngapi aumezivunja amri na sheria za Mungu, na ukafuata bushawishi wa wanadamu.

7 Kwani, tazama, haungepaswa akumwogopa mwanadamu zaidi kuliko Mungu. Ingawa wanadamu hudharau ushauri wa Mungu, na bkuyapuuza maneno yake—

8 Lakini wewe ungelipaswa kuwa mwaminifu; na yeye angelikunyooshea mkono wake na kukutegemeza dhidi ya amishale ya moto ya badui; na yeye angelikuwa pamoja na wewe katika wakati wote wa cmatatizo.

9 Tazama, wewe ndiwe Joseph, na wewe uliteuliwa kuifanya kazi ya Bwana, lakini kwa sababu ya uvunjaji wa sheria, kama hautakuwa mwangalifu, na wewe utaanguka.

10 Lakini kumbuka, Mungu ni mwenye rehema; hivyo basi, tubu kwa lile ambalo umelifanya ambalo ni kinyume cha amri ambazo nilikupa, na wewe bado u mteule, na wewe tena umeitwa kuifanya kazi;

11 Usipofanya haya, nawe utatolewa na kuwa kama watu wengine, na usiwe na kipawa zaidi.

12 Na wakati wewe ulipokitoa kile ambacho Mungu alikupa wewe kuona na uwezo wa akutafsiri, wewe ukakitoa kile ambacho kilikuwa kitakatifu na kukiweka katika mikono ya bmtu mwovu,

13 Ambaye ameyapuuza mashauri ya Mungu, na kuvunja ahadi takatifu zilizofanywa mbele za Mungu, na yeye akategemea zaidi maamuzi yake binafsi na akujivuna katika hekima yake mwenyewe.

14 Na hii ndiyo sababu ya kwamba wewe umepoteza heshima yako kwa muda—

15 Kwani wewe umeruhusu ushauri wa amkurugenzi wako ukanyagwe kutoka mwanzoni.

16 Hata hivyo, kazi yangu itaendelea mbele, kwani kadiri ufahamu wa aMwokozi ulivyokuja duniani, kupitia kwa bushuhuda wa Wayahudi, hivyo ndivyo cufahamu wa Mwokozi utakavyokuja kwa watu wangu—

17 Na kwa aWanefi, na Wayakobo, na Wayusufu, na Wazoramu, kupitia ushuhuda wa baba zao—

18 Na aushuhuda huu utakuja kujulikana kwa bWalamani, na Walemueli, na Waishmaeli, ambao cwalififia katika kutokuamini kwa sababu ya uovu wa baba zao, ambao Bwana alikubali dwawaangamize ndugu zao Wanefi, kwa sababu ya maovu yao na machukizo yao.

19 Na ni kwa asababu hii bmabamba haya yalihifadhiwa, ambayo yana kumbukumbu hizi—kwamba cahadi za Bwana ziweze kutimilika, ambazo alizifanya kwa watu wake;

20 Na kwamba aWalamani waweze kuja katika ufahamu wa baba zao, na kwamba waweze kujua ahadi za Bwana, na kwamba waweze bkuamini injili na ckutegemea fadhili za Yesu Kristo, na dkutukuzwa kwa njia ya imani katika jina lake, na kwamba kwa njia ya toba yao waweze kuokolewa. Amina.