Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 22


Sehemu ya 22

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Manchester, New York, 16 Aprili 1830. Ufunuo huu ulitolewa kwa Kanisa katika matokeo ya baadhi ya watu waliobatizwa hapo awali wakitamani kuungana na Kanisa bila ya kubatizwa tena.

1, Ubatizo ni agano jipya na lisilo na mwisho; 2–4, Ubatizo wenye mamlaka unahitajika.

1 Tazama, ninawaambia kwamba maagano yote ya azamani nimeyaondoa katika jambo hili; na hili ni agano bjipya na lisilo na mwisho, hata lile lililokuweko tangu mwanzo.

2 Kwa hivyo, hata kama mwanadamu angebatizwa mara mia haitamfaa lolote, kwani hamuwezi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba kwa atorati ya Musa, wala kwa bkazi zenu zisizo na uhai.

3 Kwani ni kwa sababu ya kazi zenu zisizo na uhai kwamba nimefanya agano hili la mwisho na kanisa hili lijengwe kwa ajili yangu, kama ilivyokuwa katika siku za kale.

4 Kwa hivyo, ingieni ninyi katika amlango, kama nilivyoamuru, na wala bmsitake kumshauri Mungu wenu. Amina.