Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 32


Sehemu ya 32

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Parley P. Pratt na Ziba Peterson, huko Manchester, New York, mapema Oktoba 1830. Shauku kubwa na hamu iliwaingia wazee hawa kuhusiana na Walamani, ambao ahadi zao zilikuwa zimetabiriwa na kufundishwa Kanisani kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni. Kama matokeo, maombi yalifanywa ili kwamba Bwana aonyeshe mapenzi yake kama wazee watumwe kwa wakati huo kwenda kwa makabila ya Wahindi hao huko Magharibi. Ufunuo huu ulifuata.

1–3, Parley P. Pratt na Ziba Peterson wanaitwa kuhubiri kwa Walamani wakiongozana na Oliver Cowdery na Peter Whitmer Mdogo; 4–5, Wanapaswa kuomba kwa ajili ya kufahamu maandiko.

1 Na sasa, kuhusu mtumishi wangu aParley P. Pratt, tazama, ninasema naye kwamba kadiri vile mimi niishivyo ninataka kwamba yeye akatangaze injili yangu na bkujifunza kutoka kwangu, na kuwa mpole na mnyenyekevu wa moyo.

2 Na lile ambalo nimemchagulia yeye ni akuongozana na watumishi wangu, Oliver Cowdery na Peter Whitmer, Mdogo, kwenda nyikani miongoni mwa bWalamani.

3 Na aZiba Peterson pia atakwenda pamoja nao; na Mimi mwenyewe nitakwenda pamoja nao na nitakuwa bkatikati yao; na cmtetezi wenu kwa Baba, na wala hakuna kitakachowashinda.

4 Nao awatayafuata yaliyoandikwa, na wala wasijisingizie bufunuo mwingine; nao wataomba daima, na niweze ckuwafunulia haya kwa dufahamu wao.

5 Na watayafuata maneno haya na hawatayapuuza. Nami nitawabariki. Amina.