Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 82


Sehemu ya 82

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii, katika Independence, Wilaya ya Jackson, Missouri, 26 Aprili 1832. Tukio hili lilikuwa la baraza kuu la makuhani wakuu na wazee wa Kanisa. Katika baraza hili, Joseph Smith alikubalika kama Rais wa Ukuhani Mkuu, ofisi ambayo hapo awali alikuwa ametawazwa katika mkutano wa makuhani wakuu, wazee, na waumini, huko Amherst, Ohio, 25 Januari 1832 (ona kichwa cha habari cha sehemu ya 75). Ufunuo huu ulirudia kusema maelekezo yaliyotolewa katika ufunuo wa awali (sehemu ya 78) wa kuanzisha kampuni—ijulikanayo kama Kampuni ya Ushirika (chini ya maelekezo ya Joseph Smith, neno “shirika” baadae lilikuja kutumika badala ya “kampuni”)—ili kutawala duka la bidhaa la Kanisa na kazi za uchapishaji.

1–4, Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakiwa vingi; 5–7, Giza latawala katika ulimwengu; 8–13, Bwana analazimika wakati tukifanya asemayo Yeye; 14–18, Sayuni lazima iongezeke katika uzuri na utakatifu; 19–24, Kila mtu yampasa kutafuta ustawi wa jirani yake.

1 Amini, amini, ninawaambia, watumishi wangu, kwamba kwa kuwa ammesameheana ninyi kwa ninyi makosa yenu, hata Mimi, Bwana, ninawasamehe.

2 Hata hivyo, kuna watu miongoni mwenu ambao wametenda dhambi kupita kiasi; ndiyo, hata ninyi anyote mmetenda dhambi; lakini amini ninawaambia, jihadharini kutoka sasa, na jiepusheni na dhambi, isije hukumu kali ikashuka juu ya vichwa vyenu.

3 Kwani yule aliyepewa avingi kwake huyo bvitatakiwa vingi; na yule caliyetenda dhambi dhidi ya dnuru kuu zaidi atapokea hukumu kuu zaidi.

4 Mlilingane jina langu kwa amafunuo, nami nitayatoa kwenu; na kadiri msivyoyashika maneno yangu, ambayo ninawapa, mnakuwa wavunjaji wa sheria; na bhaki na hukumu ni adhabu zilizowekwa kwa sheria yangu.

5 Kwa hiyo, lile nisemalo kwa mmoja ninalisema kwa wote: aKesheni, kwani badui anaeneza utawala wake, na cgiza linatawala;

6 Na hasira ya Mungu inawaka dhidi ya wakazi wa dunia; na hakuna mtenda mema, kwani wote awamepotoka.

7 Na sasa, amini ninawaambia, Mimi, Bwana, sitawahesabia adhambi kwa makosa yenu; enendeni zenu na msitende dhambi tena; lakini bdhambi za awali zitamrudia yule atakayetenda dhambi tena, asema Bwana Mungu wenu.

8 Na tena, ninawaambia, ninawapa amri ampya, ili muweze kufahamu mapenzi yangu kwenu;

9 Au, kwa maneno mengine, ninatoa kwenu maelekezo jinsi ya kuweza akutenda mbele zangu, ili iweze kugeuka kwenu kwa ajili ya wokovu wenu.

10 Mimi, Bwana, aninalazimika wakati ninyi mnapofanya ninayosema; lakini msipofanya ninayosema, ninyi hamna ahadi.

11 Kwa hiyo, amini ninawaambia, kuwa ni muhimu kwa watumishi wangu Edward Partridge na Newel K. Whitney, A. Sidney Gilbert na Sidney Rigdon, na mtumishi wangu Joseph Smith, na John Whitmer na Oliver Cowdery, na W. W. Phelps na Martin Harris wafungwe apamoja kwa mkataba na agano ambalo haliwezi kuvunjika kwa kuvunja sheria, isipokuwa hukumu imefuata mara moja, katika usimamizi wenu mbalimbali—

12 Kusimamia masuala ya maskini, na mambo yote yahusianayo na uaskofu kote katika nchi ya Sayuni na katika nchi ya Kirtland;

13 Kwani nimeiweka wakfu nchi ya Kirtland katika wakati wangu mwenyewe kwa faida ya watakatifu wa Aliye Juu Sana, na kwa ajili ya akigingi kwa Sayuni.

14 Kwani Sayuni lazima iongezeke katika uzuri, na katika utakatifu; mipaka yake lazima ipanuliwe; na vigingi vyake lazima viimarishwe; ndiyo, amini ninawaambia, aSayuni lazima ichomoze na kuvaa bmavazi yake mazuri.

15 Kwa hiyo, ninatoa kwenu amri hii, kuwa jifungeni wenyewe kwa agano hili, na ifanyike kulingana na sheria za Bwana.

16 Tazama, na hii pia ndiyo hekima kwangu kwa faida yenu.

17 Nanyi mnapaswa kuwa asawa, au kwa maneno mengine, mtakuwa na haki sawa juu ya mali, kwa ajili ya kusaidia kusimamia masuala yahusuyo usimamizi wenu, kila mtu kulingana na mahitaji na matakwa yake, ilimradi matakwa yake, ni ya haki—

18 Na hii yote ni kwa manufaa ya kanisa la Mungu aliye hai, ili kila mtu aweze kuongeza talanta yake, ili kila mtu aweze kuongeza atalanta zingine, ndiyo, hata mara mia, ambazo zinawekwa katika bghala ya Bwana, na kuwa mali ya jumuiya ya kanisa lote—

19 Kila mtu akitafuta ustawi wa jirani yake, na kufanya mambo yote akwa ajili ya utukufu wa Mungu.

20 aUtaratibu huu nimeuteua ili uwe utaratibu usio na mwisho kwenu ninyi, na kwa warithi wenu, ilimradi kama hamtatenda dhambi.

21 Na mtu atakayetenda dhambi kinyume na agano hili, na kuushupaza moyo wake dhidi ya hilo, alishughulikiwa kulingana na sheria za kanisa langu, atatolewa kwa akaramu ya Shetani hadi siku ya ukombozi.

22 Na sasa, amini ninawaambia, na hii ndiyo hekima, jifanyeni marafiki kwa mali ya udhalimu, nao hawatawaangamiza.

23 Niachieni hukumu mimi peke yangu, kwani ni yangu nami anitalipa: Amani na iwe kwenu; baraka zangu zitaendelea kuwa nanyi.

24 Kwani aufalme bado ni wenu, na utakuwa nanyi hata milele, kama hamtaanguka kutoka uimara wenu. Hivyo ndivyo. Amina.