Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 81


Sehemu ya 81

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Hiram, Ohio, 15 Machi 1832. Frederick G. Williams anaitwa kuwa kuhani mkuu na mshauri katika Urais wa Ukuhani Mkuu. Kumbukumbu za kihistoria zinaonyesha kuwa wakati ufunuo huu ulipopokelewa mnamo Machi 1832, ulimwita Jesse Gause katika ofisi ya ushauri kwa Joseph Smith katika Urais. Hata hivyo, aliposhindwa kuendelea katika mwenendo sahihi sawa na uteuzi huu, wito huu baadaye ulihamishiwa kwa Frederick G. Williams. Ufunuo huu (wa Machi 1832) uchukuliwe kama ni hatua muhimu ya kuelekea kwenye mfumo rasmi wa Urais wa Kwanza, wito maalumu wa ofisi ya mshauri katika baraza hilo na kuelezea heshima ya uteuzi huu. Ndugu Gause alitumikia kwa muda lakini alitengwa na Kanisa Desemba 1832. Ndugu Williams alitawazwa katika ofisi hii 18 Machi 1833.

1–2, Funguo za ufalme daima zinashikiliwa na Urais wa Kwanza; 3–7, Kama Frederick G. Williams ni mwaminifu katika huduma yake, atapata uzima wa milele.

1 Amini, amini, ninakuambia wewe mtumishi wangu Frederick G. Williams: Sikiliza sauti yake anenaye, neno la Bwana Mungu wako, na usikilize wito ambao umeitiwa, hata kuwa akuhani mkuu katika kanisa langu, na mshauri kwa mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo;

2 Kwake yeye nimetoa afunguo za ufalme, ambazo daima ni za bUrais wa Ukuhani Mkuu.

3 Kwa hiyo, amini ninamtambua na nitambariki yeye, na wewe pia, kadiri wewe utakavyokuwa mwaminifu katika ushauri, katika ofisi ambayo nimekuteua, kwa sala daima, kwa sauti na katika moyo wako, hadharani na faraghani, pia katika huduma yako katika kuitangaza injili katika nchi ya walio hai, na miongoni mwa ndugu zako.

4 Na katika kufanya mambo haya utakuwa umefanya mema makuu kwa wanadamu wenzako, na utakuwa umeukuza autukufu wake aliye Bwana wako.

5 Kwa hiyo, uwe mwaminifu; simama katika ofisi ambayo nimekuteua; awasaidie wadhaifu, inyooshe mikono iliyolegea, na byaimarishe magoti yaliyo cdhaifu.

6 Na kama utakuwa mwaminifu hadi mwisho nawe utapata tuzo la amwili usiokufa, na buzima wa milele katika cmakao ambayo nimeyatayarisha katika nyumba ya Baba yangu.

7 Tazama, na lo, haya ndiyo maneno ya Alfa na Omega, hata Yesu Kristo. Amina.