Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 105


Sehemu ya 105

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, kando ya Mto Fishing, Missouri, 22 Juni 1834. Chini ya uongozi wa Nabii, Watakatifu kutoka Ohio na maeneo mengine walitembea kwa miguu kwenda Missouri katika msafara ambao baadae ulijulikana kama Kambi ya Sayuni. Madhumuni yao yakiwa ni kuwasindikiza Watakatifu wa Missouri waliofukuzwa warudi katika ardhi yao huko Wilaya ya Jackson. Wamisouri ambao hapo awali waliwatesa Watakatifu waliogopa ulipaji kisasi kutoka kwa Kambi ya Sayuni na kwa kushtukiza wakawahi kuwashambulia Watakatifu wanaoishi katika Wilaya ya Clay, huko Missouri. Baada ya gavana wa Missouri kufuta ahadi yake ya kuwasaidia Watakatifu, Joseph Smith alipokea ufunuo huu.

1–5, Sayuni itajengwa kulingana na sheria ya selestia; 6–13, Ukombozi wa Sayuni unacheleweshwa kwa kipindi kifupi; 14–19, Bwana atapigana vita vya Sayuni; 20–26, Watakatifu watakuwa wenye hekima na wala wasijivunie matendo makuu wakati wanapokusanyika; 27–30, Ardhi katika Jackson na wilaya zinazopakana nayo lazima inunuliwe; 31–34, Wazee watapokea endaomenti katika nyumba ya Bwana katika Kirtland; 35–37, Watakatifu ambao wameitwa na kuteuliwa watatakaswa; 38–41, Watakatifu watainua bendera ya amani kwa walimwengu.

1 Amini ninawaambia mliojikusanya pamoja ili mpate kujifunza mapenzi yangu juu ya aukombozi wa watu wangu walioteseka—

2 Tazama, ninawaambia, kama isingekuwa auvunjaji wa sheria wa watu wangu, nikizungumza juu ya kanisa na siyo mtu mmoja mmoja, wangelikuwa wamekwisha kombolewa hata sasa.

3 Lakini tazama, hawajajifunza kuwa watiifu kwa mambo ambayo ninayataka kutoka kwao, bali wamejaa aina zote za uovu, wala ahawagawi mali zao, kama iwapasavyo watakatifu, kwa maskini na walioteseka miongoni mwao;

4 Na hawana aushirikiano kulingana na ushirika unaotakiwa kwa sheria ya ufalme wa selestia;

5 Na aSayuni haiwezi kujengwa bisipokuwa kwa kanuni ya csheria ya ufalme wa selestia; vinginevyo siwezi kumpokea kwangu.

6 Na watu wangu hawanabudi akurudiwa hadi wajifunze butii, kama ni lazima, kwa mambo ambayo wanateseka.

7 Mimi sisemi juu ya wale walioteuliwa kuwaongoza watu wangu, ambao ni wazee wa akwanza wa kanisa langu, kwani siyo wote walio chini ya hatia hii;

8 Bali ninazungumzia juu ya makanisa yangu yaliyoko ngʼambo—wako wengi watakaosema: Mungu wao yuko wapi? Tazama, atawaokoa katika wakati wa taabu, vinginevyo hatutakwenda Sayuni, na tutazishikilia fedha zetu.

9 Kwa hiyo, kwa sababu ya auvunjaji wa sheria wa watu wangu, ni muhimu kwangu kwamba wazee wangu lazima wasubiri kwa kipindi kifupi kwa ajili ya ukombozi wa Sayuni—

10 Ili wao wenyewe wapate kujitayarisha, na ili watu wangu wapate kufundishwa kiukamilifu zaidi, na kupata uzoefu, na kujua kiukamilifu awajibu wao, na mambo niyatakayo kutoka kwao.

11 Na hii haiwezi kutimia hadi awazee wangu wamepewa bendaomenti kutoka juu.

12 Kwani tazama, nimetayarisha endaomenti kubwa na baraka azitakazomwagwa juu yao, kadiri watakavyokuwa waaminifu na kuendelea katika unyenyekevu mbele zangu.

13 Kwa hiyo ni muhimu kwangu kwamba wazee wangu lazima wasubiri kwa kipindi kifupi, kwa ajili ya ukombozi wa Sayuni.

14 Kwani tazama, sihitaji kutoka kwao kupigana vita vya Sayuni; kama nilivyosema katika amri ya zamani, hata hivyo, nitatimiza—anitapigana vita vyenu.

15 Tazama, amwangamizi nimemtuma kuangamiza na kuwaharibu adui zangu; na siyo miaka mingi kutoka sasa hawataachwa kuuchafua urithi wangu, na bkulidharau jina langu juu ya nchi ambayo nimeiweka cwakfu kwa ajili ya kukusanywa pamoja kwa watakatifu wangu.

16 Tazama, nimemwamuru mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, kusema na anguvu ya nyumba yangu, hata mashujaa wangu, vijana wangu, na walio wa umri wa kati, kujikusanya pamoja kwa ajili ya ukombozi wa watu wangu, na kuitupa chini minara ya adui zangu, na kuwatawanya bwalinzi wao;

17 Lakini nguvu za nyumba yangu haijatii maneno yangu.

18 Lakini ilimradi wapo wale ambao wameyatii maneno yangu, nimewatayarishia baraka na aendaomenti, kama wataendelea kuwa waaminifu.

19 Nimezisikia sala zao, na nitayapokea matoleo yao; na ni muhimu kwangu kwamba lazima wafikishwe mbali hivyo kwa ajili ya kujaribiwa kwa aimani yao.

20 Na sasa, amini ninawaambia, amri ninaitoa kwenu, kwamba kama vile wengi walivyokuja hapa, ambao wanaweza kukaa katika maeneo ya jirani, acheni wakae;

21 Na wale wasioweza kukaa, ambao wanazo familia huko mashariki, acheni wakae kwa kipindi kifupi, kadiri mtumishi wangu Joseph Smith atakavyowapangia;

22 Kwani nitamshauri juu ya jambo hili, na mambo yote yale atakayowapangia yatatimizwa.

23 Na acheni watu wangu wote wakaao katika maeneo ya jirani wawe waaminifu sana, na wenye kuomba, na wanyenyekevu mbele zangu, na wasifichue mambo ambayo nimewafunulia wao, hadi itakapokuwa hekima kwangu kwamba wayafichue.

24 Msizungumzie hukumu, wala amsijivunie imani wala matendo makuu, bali kusanyikeni pamoja kwa uangalifu, iwezekanavyo katika eneo moja kadiri itakavyokubalika katika hisia za watu;

25 Na tazama, nitakupeni ninyi fadhili na neema machoni mwao, ili mpate kupumzika katika aamani na usalama, wakati mkisema kwa watu hawa: Tufanyieni hukumu na haki kwa ajili yetu kulingana na sheria, na tufidieni kwa mabaya mliyotutendea.

26 Sasa, tazama, ninawaambia, marafiki zangu, kwa njia hii muweze kupata fadhili machoni mwa watu hawa, hadi ajeshi la Israeli litakapokuwa kubwa sana.

27 Nami nitailainisha mioyo ya watu hawa, kama nilivyoufanya moyo wa aFarao, mara kwa mara, hadi mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na wazee wangu, ambao nimewateua, wapate muda wa kuikusanya nguvu ya nyumba yangu,

28 Na kuwatuma watu wenye ahekima, kukamilisha yale niliyoamuru juu ya bkununua ardhi yote katika wilaya ya Jackson ile iwezekanayo kununuliwa, na katika wilaya zilizopo karibu.

29 Kwani ni mapenzi yangu kwamba ardhi hizi zapaswa kununuliwa; na baada ya kununuliwa kwamba watakatifu wangu wazimiliki kulingana na asheria za uwekaji wakfu ambazo nimewapatia.

30 Na baada ya ardhi hizi kununuliwa, nitayaona amajeshi ya Israeli kuwa hayana hatia katika kumiliki ardhi iliyo yao wenyewe, ambayo awali waliinunua kwa fedha yao, na kuiangusha chini minara ya adui zangu ambayo yaweza kuwa juu yao, na kuwatawanya walinzi wao, na bkunipatia haki mimi na adui zangu hata kwa kizazi cha tatu na cha nne cha wale wanichukiao.

31 Lakini kwanza acheni jeshi langu liwe kubwa sana, na acheni alitakaswe mbele yangu, ili lipate kuwa zuri kama jua, na safi kama bmwezi, na kwamba bendera zake ziwe za kutisha kwa mataifa yote;

32 Ili falme za ulimwengu huu zipate kulazimishwa kutambua kwamba ufalme wa Sayuni hakika ni aufalme wa Mungu wetu na Kristo wake, kwa hiyo, na btujiweke chini ya sheria zake.

33 Amini ninawaambia, ni muhimu kwangu kwamba wazee wa kwanza wa kanisa langu wapokee aendaomenti kutoka juu katika nyumba yangu, ambayo nimeamuru ijengwe katika jina langu katika nchi ya Kirtland.

34 Na amri zile ambazo nimewapa juu ya Sayuni na asheria yake zitelekezwe na kutimizwa, baada ya ukombozi wake.

35 Palikuwa na siku ya akuitwa, lakini wakati umefika wa siku ya kuteua; na acha wale watakaoteuliwa wawe wenye bkustahili.

36 Na itajulishwa kwa mtumishi wangu, kwa sauti ya Roho, wale awalioteuliwa; nao bwatatakaswa;

37 Na kadiri watakavyofuata aushauri ambao wanaupokea, watakuwa na uwezo baada ya siku nyingi wa kukamilisha mambo yote yahusuyo Sayuni.

38 Na tena ninawaambia, fungueni mashtaka kwa ajili ya amani, siyo tu kwa watu ambao wamewapiga peke yake, bali pia kwa watu wote;

39 Na inueni abendera ya bamani, na tengenezeni tangazo la amani hata kwenye miisho ya dunia;

40 Na toeni mapendekezo kwa ajili ya amani kwa wale walio wapiga, kulingana na sauti ya Roho aliye ndani yenu, na mambo ayote yatafanya kazi kwa pamoja kwa faida yenu.

41 Kwa hiyo, kuweni waaminifu; na tazama, na lo, aMimi nipo pamoja nanyi hadi mwisho. Hivyo ndivyo. Amina.