Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 37


Sehemu ya 37

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii na Sidney Rigdon, karibu na Fayette, New York, Desemba 1830. Katika hii sehemu kumetolewa amri ya kwanza kuhusu kukusanyika katika kipindi hiki.

1–4, Watakatifu wanaitwa kukusanyika huko Ohio.

1 Tazama, ninawaambia kuwa haina manufaa kwangu mimi kwamba ninyi mwendelee akutafsiri zaidi hadi mtakapokwenda Ohio, na hii ni kwa sababu ya adui na faida yenu ninyi.

2 Na tena, ninawaambia kuwa msiende mpaka mtakapokuwa mmehubiri injili yangu katika sehemu zile, na kuliimarisha kanisa popote linapopatikana, na zaidi katika aColesville; kwani, tazama, wanaomba kwangu katika imani kubwa.

3 Na tena, amri ninaitoa kwa kanisa, kwamba ni kwa manufaa kwangu mimi kuwa yawapasa kukusanyika pamoja huko aOhio, katika wakati ambao mtumishi wangu Oliver Cowdery atakaporejea kwao.

4 Tazama, hii ni hekima, na acha kila mtu aajichagulie mwenyewe hadi nitakapokuja. Hivyo ndivyo. Amina.