Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 39


Sehemu ya 39

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa James Covel, huko Fayette, New York, 5 Januari 1831. James Covel ambaye alikuwa mchungaji wa Kimethodisti kwa karibu miaka arobaini, aliagana na Bwana kuwa atatii amri yoyote ambayo Bwana atampa kupitia Joseph Nabii.

1–4, Watakatifu wanao uwezo wa kuwa wana wa Mungu; 5–6, Kuipokea injili ni kumpokea Kristo; 7–14, James Covel anaamriwa kubatizwa na kufanya kazi katika shamba la mizabibu la Bwana; 15–21, Watumishi wa Bwana wataihubiri injili kabla ya Ujio wa Pili; 22–24, Wale ambao huipokea injili watakusanyika wakati huu na hata milele.

1 Sikiliza na sikia sauti yake yeye aliye wa kutoka amilele hadi milele yote; bMimi Ndimi Mkuu, hata Yesu Kristo—

2 aNuru na uzima wa ulimwengu; nuru ingʼaayo gizani na hata giza haikuitambua;

3 Yeye yule ambaye alikuja awakati wa meridiani alikuja kwa walio wangu, na walio wangu hawakunipokea;

4 Bali wote walionipokea, niliwapa uwezo wa kufanyika awana wangu; na vivyo hivyo nitawapa wale wote wanipokeao Mimi, uwezo wa kufanyika wana wangu.

5 Na amini, amini ninakuambia, yeye aipokeaye injili yangu aanipokea Mimi, na yeye asiyeipokea injili yangu hanipokei Mimi.

6 Na hii ni ainjili yangu—toba na ubatizo wa maji, na halafu huja bubatizo wa moto na Roho Mtakatifu, hata Mfariji, aonyeshaye mambo yote, na cafundishaye mambo ya amani yaliyo ya ufalme.

7 Na sasa, tazama, ninakuambia, mtumishi wangu aJames, nimeziangalia kazi zako na ninakujua wewe.

8 Na amini, ninakuambia, moyo wako sasa ni mnyoofu mbele zangu kwa wakati huu; na, tazama, nimeweka baraka kubwa juu ya kichwa chako;

9 Hata hivyo, wewe umeona huzuni kuu, kwa kuwa umenikataa mimi mara nyingi kwa sababu ya kiburi na shughuli za aulimwengu.

10 Lakini, tazama, siku za ukombozi wako zimefika, kama utaisikiliza sauti yangu, ambayo yasema kwako wewe: Simama na aubatizwe, na ukaoshe dhambi zako, ukilingana jina langu, nawe utampokea Roho wangu, na baraka kubwa namna hii ambayo kamwe hujazijua.

11 Na kama wewe utafanya haya, nimekutayarisha kwa ajili ya kazi kuu. Wewe utahubiri utimilifu wa injili yangu, ambayo nimeileta katika siku hizi za mwisho, agano ambalo nimelileta ili akuwarejesha watu wangu, ambao ni wa nyumba ya Israeli.

12 Na itakuwa kwamba uwezo autakuwa juu yako; utakuwa na imani kubwa, na Mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitatangulia mbele ya uso wako.

13 Na umeitwa akufanya kazi katika shamba langu la mizabibu, na kulijenga kanisa langu, na bkuistawisha Sayuni, ili kwamba iweze kufurahi juu ya vilima na ckustawi.

14 Tazama, amini, amini, ninakuambia, hujaitwa kwenda katika nchi za mashariki, bali umeitwa kwenda Ohio.

15 Na kadiri watu wangu watakavyokusanyika wenyewe kule Ohio, nimeweka katika ghala abaraka ambayo haijapata kujulikana miongoni mwa wanadamu, nayo itamiminwa juu ya vichwa vyao. Na kutokea huko watu watakwenda katika bmataifa cyote.

16 Tazama, amini, amini, ninakuambia, kwamba watu huko Ohio wananilingana katika imani kubwa, wakifikiria kuwa nitauzuia mkono wangu katika hukumu juu ya mataifa, lakini siwezi kulikana neno langu.

17 Kwa hiyo anza kazi kwa nguvu zako zote na waite wafanyakazi waaminifu katika shamba langu la mizabibu, ili liweze akupogolewa kwa mara ya mwisho.

18 Na kadiri watakavyotubu na kupokea utimilifu wa injili yangu, na kutakaswa, nitauzuia mkono wangu katika ahukumu.

19 Kwa hivyo, nenda, ukipaza sauti kubwa, ukisema: Ufalme wa mbingu u karibu; paza sauti, ukisema: Hosana! libarikiwe jina la Mungu Aliye Juu Sana.

20 Nenda na ukabatize kwa maji, ukiitengeneza njia mbele ya uso wangu kwa ajili ya wakati wa aujio wangu;

21 Kwani wakati umekaribia; asiku wala saa hakuna bajuaye; bali hakika yaja.

22 Na yeye ayapokeaye mambo haya anipokea Mimi; na watakusanyika kwangu sasa na hata milele.

23 Na tena, na itakuwa kwamba juu ya wote utakaowabatiza kwa maji, utawawekea amikono yako, na watapokea bkipawa cha Roho Mtakatifu, na cwatatazamia ishara za dujio wangu, na watanijua.

24 Tazama, naja haraka. Hivyo ndivyo. Amina.