Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 51


Sehemu ya 51

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii huko Thompson, Ohio, 20 Mei 1831. Kwa wakati huu watakatifu wanaohamia kutoka mashariki walianza kufikia Ohio, na ilikuja kuwa muhimu kufanya mipango ya makazi yao. Na kazi hii ilikuwa wajibu wa ofisi ya askofu, Askofu Edward Partridge aliomba mwongozo juu ya jambo hili, na hivyo Nabii alimwomba Bwana.

1–8, Edward Partridge ameteuliwa kudhibiti usimamizi na mali; 9–12, Watakatifu lazima wafanyiane haki na kupokea sawa sawa; 13–15, Ni lazima wawe na ghala ya askofu na kupanga mali kulingana na sheria ya Bwana; 16–20, Ohio patakuwa mahali pa kukusanyika kwa muda.

1 Nisikilizeni Mimi, asema Bwana Mungu wenu, na nitasema naye mtumishi wangu aEdward Partridge, na kumpa yeye maelekezo; kwani ni muhimu kwamba apokee maelekezo namna ya kuwasimamia watu hawa.

2 Kwani ni muhimu kwamba wasimamiwe kulingana na asheria zangu; vinginevyo, watakatiliwa mbali.

3 Kwa hivyo, mtumishi wangu Edward Partridge, na wale aliowateua, ambao ninapendezwa nao, wawagawie watu hawa sehemu zao, kila mtu asawa kulingana na familia yake, na kulingana na hali yake na matakwa na bshida zake.

4 Na mtumishi wangu Edward Partridge, wakati atakapomgawia mtu sehemu yake, na ampe hati ambayo itahakikisha kuwa ni sehemu yake, kwamba ataishikilia hati hiyo na urithi huu katika kanisa, hadi avunje sheria na kutohesabiwa kustahili kwa sauti ya kanisa, kulingana na sheria na amaagano ya kanisa, juu ya ustahiki kanisani.

5 Na kama atavunja sheria na hahesabiwi kuwa mwenye kustahili kuwa katika kanisa, hatakuwa na uwezo wa kudai ile sehemu ambayo aliyoiweka wakfu kwa askofu kwa ajili ya maskini na wenye shida wa kanisa langu; kwa hiyo, hatarejeshewa zawadi hiyo, bali atakuwa na madai tu ya sehemu ile aliyogawiwa yeye.

6 Na hivyo ndivyo mambo yote yatakavyolindwa, akulingana na bsheria za nchi.

7 Na hivyo kile kilicho cha watu hawa kigawanywe kwa watu hawa.

8 Na afedha zilizosalia kwa watu hawa—na pateuliwe wakala kwa watu hawa, na kuchukua bfedha hizo kwa ajili ya kuleta vyakula na mavazi, kulingana na mahitaji ya watu hawa.

9 Na kila mtu na afanye ahaki, na kuwa sawa miongoni mwa watu hawa, na kupokea sawa, ili kwamba muweze kuwa na bumoja, kama vile nilivyowaamuru.

10 Na kile kilicho cha watu hawa kisichukuliwe na kutolewa kwa wale wa akanisa jingine.

11 Kwa hiyo, kama kanisa jingine watapokea fedha za kanisa hili, na walipe kwa kanisa hili tena kulingana na makubaliano yao;

12 Na hii itafanyika kupitia kwa askofu au wakala, ambaye atateuliwa kwa asauti ya kanisa.

13 Na tena, na askofu ataanzisha aghala kwa kanisa hili; na mambo yote ya fedha na katika vyakula, ambayo ni zaidi ya bmahitaji kwa watu hawa, vitunzwe katika mikono ya askofu.

14 Na yeye pia ajiwekee kwa mahitaji yake yeye mwenyewe, na kwa mahitaji ya familia yake, tangu atakapoajiriwa katika kufanya shughuli hii.

15 Na hivyo ndivyo ninavyowapa watu hawa nafasi ya kujisimamia wenyewe kulingana na asheria zangu.

16 Nami ninaiweka wakfu anchi hii kwa ajili yao kwa majira mafupi, hadi Mimi, Bwana, nitakapopanga vinginevyo, na kuwaamuru kwenda kutoka hapa;

17 Na saa wala siku haijatolewa kwao, kwa hiyo wafanye katika nchi hii kana kwamba wapo kwa miaka mingi, na hii itageuka kuwa vyema kwao.

18 Tazama, huu utakuwa ni amfano kwa mtumishi wangu Edward Partridge, katika mahali pengine, katika makanisa yote.

19 Na yeyote atakayepatikana kuwa mwaminifu, mwenye haki, na amtumishi mwenye hekima ataingia katika bshangwe ya Bwana wake, na ataurithi uzima wa milele.

20 Amini, ninawaambia, Mimi ndimi Yesu Kristo, anaja upesi, katika bsaa msiyodhani. Hivyo ndivyo. Amina.