Sehemu ya 116
Dondoo kutoka kwenye historia ya Joseph Smith ikisimulia ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii, karibu na Kivuko cha Wight, mahali paitwapo Spring Hill, Wilaya ya Daviess, Missouri, Mei au Juni 1838.
1 Spring Hill Bwana alipaita Adamu-ondi-Amani, kwa sababu, alisema, ndipo mahali ambapo Adamu atakuja kuwatembelea watu wake, au Mzee wa Siku atakapokaa, kama ilivyonenwa na Danieli nabii.