Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 8


Sehemu ya 8

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Oliver Cowdery, huko Harmony, Pennsylvania, Aprili 1829. Katika mpangilio wa kutafsiri Kitabu cha Mormoni, Oliver, ambaye aliendelea kutumika kama mwandishi, kuandika imla iliyokuwa ikitafsiriwa na Nabii, alitamani kupewa kipawa cha tafsiri. Bwana alijibu maombi yake kwa kumpa ufunuo huu.

1–5, Ufunuo huja kwa uwezo wa Roho Mtakatifu; 6–12, Maarifa ya siri za Mungu na uwezo wa kutafsiri kumbukumbu za kale huja kwa imani.

1 aOliver Cowdery, amini, amini, ninakuambia, kwamba hakika kama Bwana aishivyo, ambaye ndiye Mungu na Mkombozi wako, hata hivyo hakika waweza nawe kupata bmaarifa ya chochote kile cutakachokiomba kwa imani, na moyo mnyoofu, ukiamini kwamba utapata maarifa kuhusiana na michoro ya dkumbukumbu ya zamani, ambayo ni ya kale, ambayo ndani yake mna sehemu zile za andiko langu ambalo limezungumziwa kwa eufunuo wa Roho wangu.

2 Ndiyo, tazama, anitakujulisha wewe akilini mwako na katika bmoyo wako, kwa njia ya cRoho Mtakatifu, ambaye atakujia na ambaye atakaa moyoni mwako.

3 Sasa, tazama, hii ndiyo roho ya ufunuo; tazama, huyu ndiye Roho ambaye kwa yeye Musa aliwaongoza wana wa Israeli kupitia aBahari ya Shamu kwenye nchi kavu.

4 Hivyo basi hiki ni kipawa chako; kitumie, na umebarikiwa wewe, kwani kitakukomboa wewe kutoka katika mikono ya adui zako, wakati, kama isingalikuwa hivyo, wangelikuua wewe na kuiweka nafsi yako kwenye uharibifu.

5 O, kumbuka amaneno haya, na zishike amri zangu. Kumbuka, hiki ndicho kipawa chako.

6 Sasa hiki sicho kipawa pekee ulichonacho; kwani unacho kipawa kingine, ambacho ni kipawa cha Haruni; tazama, kimekuambia mambo mengi;

7 Tazama, hakuna nguvu nyingine, ila nguvu ya Mungu, ambayo yaweza kusababisha nguvu hii ya Haruni ikawa kwako wewe.

8 Hivyo basi, usitie shaka, kwani ni kipawa cha Mungu; na wewe utakishika katika mikono yako, na kufanya kazi za ajabu; na hakuna nguvu itakayoweza kuipokonya kutoka katika mikono yako, kwani hiyo ni kazi ya Mungu.

9 Na, kwa hiyo, chochote utakachoomba kwangu nikuambie kwa njia hiyo, hicho nitakupa, na utakuwa na maarifa kuhusu hilo.

10 Kumbuka kwamba pasipo aimani huwezi kufanya lolote; hivyo basi omba kwa imani. Usicheze na mambo haya; busiombe kitu kile usichopaswa kukiomba.

11 Omba kwamba wewe ujue siri za Mungu, na kwamba uweze akutafsiri na kupokea maarifa kutoka kumbukumbu zile zote za kale ambazo zimefichwa, ambazo ni takatifu; na kulingana na imani yako itakuwa hivyo kwako.

12 Tazama, ni mimi niliyeyasema haya; na ni, Mimi yule yule niliyesema na wewe kutoka mwanzo. Amina.