Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 128


Sehemu ya 128

Waraka kutoka kwa Joseph Smith Nabii kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, wenye maelekezo zaidi juu ya ubatizo kwa ajili ya wafu, ulioandikwa huko Nauvoo, Illinois, 6 Septemba 1842.

1–5, Waandishi wa maeneo na waandishi wakuu ni lazima wathibitishe ukweli wa ubatizo huo kwa ajili ya wafu; 6–9, Kumbukumbu zao zinafunga na zinaandikwa duniani na mbinguni; 10–14, Kisima cha ubatizo ni mfano wa kaburi; 15–17, Eliya alirejesha uwezo juu ya ubatizo wa wafu; 18–21, Vyote funguo, uwezo, na mamlaka za vipindi vilivyopita vimerejeshwa; 22–25, Habari njema na tukufu zimetangazwa kwa walio hai na wafu.

1 Kama nilivyoeleza kwenu katika barua yangu kabla ya kuondoka nyumbani kwangu, kwamba nitawaandikia mara kwa mara na kuwapa habari juu ya mambo mengi, sasa ninaanza tena na jambo la aubatizo kwa ajili ya wafu, kwa vile jambo hilo laonekana kutawala akili yangu, na linajisukuma kwenye hisia zangu kwa nguvu, tangu nilipokuwa nikifukuzwa na adui zangu.

2 Niliwaandikia maneno machache ya ufunuo juu ya mwandishi. Nimepata kuwa na maoni machache ya nyongeza juu ya jambo hili, ambayo sasa ninayathibitisha. Kwamba ilielezwa katika barua yangu iliyopita kwamba lazima pawepo na amwandishi, ambaye ni lazima awe shahidi wa kuona, na pia kusikia kwa masikio yake, ili apate kumbukumbu ya kweli mbele za Bwana.

3 Sasa, kuhusu jambo hili, itakuwa vigumu sana kwa mwandishi mmoja kuwepo wakati wote, na kufanya shughuli zote. Ili kuepuka tatizo hili, yawezekana kuwa mwandishi ateuliwe katika kila wadi katika mji, ambaye ana uwezo wa kuandika kumbukumbu kwa ufasaha; na acheni awe makini na sahihi katika kuandika matukio yote, akihakikisha katika maandishi yake kwamba aliona kwa macho yake, na kusikia kwa masikio yake, akitoa tarehe, na majina, na kadhalika, na historia ya shughuli yote; akitaja pia majina ya watu watatu waliopo, kama watakuwepo, ambao wanaweza kwa wakati wowote ikiwa wataitwa juu ya kuthibitisha jambo hilo hilo, ili katika vinywa vya amashahidi wawili au watatu kila neno lipate kuthibitishwa.

4 Halafu, acheni awepo mwandishi mkuu, ambaye kwake kumbukumbu hizi zinaweza kupelekwa, zikipelekwa pamoja na hati zenye saini zao wenyewe, zikithibitisha kwamba kumbukumbu ile waliyoyaandika ni ya kweli. Ndipo mwandishi mkuu wa kanisa anaweza kuingiza katika kitabu kikuu cha kanisa, pamoja na hati hizo na majina ya mashahidi wote waliokuwepo, pamoja na maelezo yake mwenyewe kwamba hakika yeye anaamini maelezo yaliyoandikwa hapo juu na anayeandika kuwa ni ya kweli, kutokana na ufahamu wake wa tabia ya jumla na kuteuliwa kwa watu wale na kanisa. Na ikiwa haya yamefanyika kwenye kitabu kikuu cha kanisa, maandiko haya yatakuwa ya haki na matakatifu, na yatafanya ibada hiyo kuwa hivyo hivyo kama vile yeye ameona kwa macho yake na kusikia kwa masikio yake, na kuiandika kumbukumbu hiyo kwenye kitabu kikuu cha kanisa.

5 Ninyi pengine mnaweza kudhani utaratibu huu wa mambo kuwa ni mrefu sana; lakini acha niwaeleze ya kuwa hii ni kujibu tu mapenzi ya Mungu, kwa kufuata maagizo na matayarisho ambayo Bwana ameagiza na kutayarisha kabla ya kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu, kwa ajili ya awokovu wa wafu ambao watakufa bila bkuifahamu injili.

6 Na zaidi, ninataka ninyi mkumbuke kwamba Yohana Mfunuzi alikuwa akitafakari juu ya jambo hili hili la wafu, wakati alipotangaza, kama mnavyoona imeandikwa katika Ufunuo 20:12Na niliwaona wafu, wadogo na wakubwa, wamesimama mbele za Mungu; na vitabu vimefunguliwa; na kitabu kingine kilifunguliwa, ambacho ni kitabu cha uzima; na wafu walihukumiwa kutokana na mambo yale yaliyoandikwa ndani ya vitabu hivi, kulingana na matendo yao.

7 Mtagundua katika dondoo hii kwamba vitabu vilifunguliwa; na kitabu kingine kilifunguliwa, ambacho kilikuwa ni akitabu cha uzima; lakini wafu walihukumiwa kutokana na mambo yaliyoandikwa ndani ya vitabu hivyo, kulingana na matendo yao; kwa hiyo, vitabu vilivyozungumzwa lazima viwe ni vitabu ambavyo vina kumbukumbu ya matendo yao, na inaonyesha kuwa ni bkumbukumbu ambazo zinatunzwa duniani. Na kitabu kilichokuwa kitabu cha uzima ni kumbukumbu inayotunzwa mbinguni; kanuni hii inakubaliana sawa sawa na mafundisho mnayoamriwa ninyi katika ufunuo uliomo katika barua ambayo nimewaandikia kabla sijaondoka nyumbani kwangu—ili katika kumbukumbu zenu zote mwandikazo ziweze kuandikwa mbinguni.

8 Sasa, kiini cha ibada hii kinategemea katika auwezo wa ukuhani, kupitia ufunuo wa Yesu Kristo, ambao ndani yake imetolewa kwamba lolote utakalolifunga duniani litafungwa mbinguni, na lolote butakalolifungua duniani litafunguliwa mbinguni. Au, kwa maneno mengine, mtazamo tofauti wa tafsiri hii, lolote utakaloliandika duniani litaandikwa mbinguni, na lolote usiloliandika duniani halitaandikwa mbinguni; kwani kutoka kwenye vitabu wafu wenu watahukumiwa, kulingana na matendo yao wenyewe, iwe wao wenyewe wametenda cibada hizo wao wenyewe, au kwa njia ya wawakilishi wao, kulingana na agizo ambalo Mungu amelitayarisha kwa ajili ya dwokovu wao tangu kabla ya kuwekwa msingi wa dunia, kulingana na kumbukumbu walizoziandika juu ya wafu wao.

9 Yawezekana kwa wengine ikaonekana ni mafundisho yasiyo ya kawaida ambayo tunayazungumzia—uwezo ambao huandika au kufunga duniani na kufungwa mbinguni. Hata hivyo, katika umri wote wa ulimwengu, wakati wowote Bwana alipokuwa ametoa akipindi cha ukuhani kwa mtu yeyote kwa ufunuo halisi, au kwa kundi lolote la wanadamu, uwezo huu daima umekuwa ukitolewa. Kwa sababu hiyo, lolote watu wale walilolifanya katika bmamlaka, katika jina la Bwana, na wakalifanya kwa ukweli na kwa uaminifu, na kutunza kwa usahihi na uaminifu kumbukumbu hiyo, ikaja kuwa sheria duniani na mbinguni, na haikuweza kuondolewa, kulingana na maamrisho ya cYehova mkuu. Hili ni neno la kuaminiwa. Ni nani awezaye kulisikia?

10 Na tena, kama mfano mwingine, Mathayo 16:18, 19: Nami pia nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya jehanamu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni: na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.

11 Sasa siri kubwa na muhimu ya jambo hili lote, na uzuri mkuu wa juu kabisa juu ya somo lote lililoko mbele yetu, linategemea katika kupata uwezo wa Ukuhani Mtakatifu. Kwake yeye ambaye amepewa afunguo hizi hakuna ugumu wa kupata maarifa ya ukweli yahusianayo na bwokovu wa wanadamu, wote vile vile kwa ajili ya wafu na walio hai.

12 Katika hili kuna autukufu na bheshima, na ckutokufa na uzima wa milele—Agizo la ubatizo kwa maji, dkuzamishwa ndani yake ili kuwa mfano wa wafu, ili kanuni moja ipate kulingana na nyingine; kuzamishwa majini na kutoka majini ni mfano wa ufufuko wa wafu kutoka makaburini mwao; kwa sababu hiyo, agizo hili liliwekwa ili kufanya uhusiano na agizo la ubatizo kwa ajili ya wafu, ukiwa ni mfano wa wafu.

13 Kwa hiyo, akisima cha maji ya ubatizo kiliwekwa kama bmfano wa kaburi, na iliamriwa kiwe chini ya mahali ambapo walio hai wamezoea kukusanyika, ili kuwaonyesha walio hai na wafu, na ili vitu vyote vipate kuwa na mifano yao, na ili vipate kulingana—kile kilicho cha duniani kikubaliane na kile kilicho cha mbinguni, kama vile Paulo alivyotangaza, 1 Wakorintho 15:46, 47, na 48:

14 Lakini hautangulii ule wa kiroho, bali ule wa kiasili; na baadaye huja ule wa kiroho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo; mtu wa pili ni Bwana atoka mbinguni. Kama alivyo yeye wa udongo ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni ndivyo walivyo pia walio wa mbinguni. Na kama zilivyo kumbukumbu duniani juu ya wafu wenu, ambayo yameandikwa kwa uhakika, pia ndivyo yalivyo maandishi mbinguni. Huu, kwa hiyo, ni uwezo wa akuunganisha na kufunga, kulingana na njia moja ya kulielewa neno, bfunguo za ufalme, ambazo zinajumuisha funguo za cmaarifa.

15 Na sasa, wapendwa ndugu na dada zangu, acheni nikuhakikishieni kwamba kanuni hizi zihusianazo na wafu na walio hai kwamba haziwezi kupuuzwa, kwa vile zinahusu wokovu wetu. Kwa kuwa awokovu wao ni wa lazima na ni muhimu kwa wokovu wetu, kama vile Paulo asemavyo juu ya mababu—kwamba wao pasipo sisi bhawakamiliki—wala sisi hatuwezi kuwa wakamilifu pasipo wafu wetu.

16 Na sasa, kuhusu ubatizo kwa ajili ya wafu, nitakupeni dondoo nyingine ya Paulo, 1 Wakorintho 15:29: Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje, kama wafu hawafufuliwi kamwe? Kwa nini kubatizwa kwa ajili ya wao?

17 Na tena, sambamba na dondoo hii nitakupeni dondoo kutoka kwa mmoja wa manabii, ambaye macho yake yaliangalia juu ya aurejesho wa Ukuhani, utukufu utakaofunuliwa katika siku za mwisho, na kwa jinsi ya pekee jambo hili tukufu juu ya mambo yote yahusuyo injili isiyo na mwisho, nalo ni, ubatizo kwa ajili ya wafu; kwani Malaki anasema, mlango wa mwisho, mstari wa 5 na wa 6: Tazama, nitamtuma kwenu bEliya nabii kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana: Naye ataigeuza mioyo ya mababu iwaelekee watoto, na mioyo ya watoto iwaelekee mababu zao, nisije nikaja na kuipiga dunia kwa laana.

18 Ningeweza kufanya tafsiri ya awazi ya hii, lakini ni wazi vya kutosha kukidhi madhumuni yangu kama vile ilivyo. Yatosha kujua, katika jambo hili, kwamba dunia itapigwa kwa laana isipokuwa pamekuwepo na bmuunganiko wa aina fulani kati ya mababu na watoto, juu ya jambo moja au jingine—na tazama jambo hilo ni lipi? Ni cubatizo kwa ajili ya wafu. Kwani sisi pasipo wao hatuwezi kukamilika; wala wao pasipo sisi hawawezi kukamilika. Si wao wala sisi tunaoweza kukamilika bila wale waliokufa katika injili pia; kwani ni muhimu katika kuingia kwa dkipindi cha utimilifu wa nyakati, kipindi ambacho sasa kinaanza kuingia, kwamba muungano wote mzima na ulio mkamilifu, na muunganiko wa pamoja wa vipindi, na funguo, na uwezo, na utukufu yapaswa ufanyike, na kufunuliwa kutoka siku za Adamu hadi wakati huu. Na siyo hili tu, bali mambo yale ambayo kamwe hayajafunuliwa kutoka kuwekwa kwa emsingi wa ulimwengu, lakini yamefichwa kwa wenye hekima na akili, yatafunuliwa kwa watoto fwachanga na wanyonyao katika hiki, kipindi cha utimilifu wa nyakati.

19 Sasa, tunasikia nini katika injili ambayo tumeipokea? Sauti ya furaha! Sauti ya rehema kutoka mbinguni; na sauti ya aukweli kutoka duniani; habari njema kwa wafu; sauti ya furaha kwa walio hai na wafu; bhabari njema ya shangwe kuu. Jinsi gani ilivyo mizuri juu ya milima cmiguu ya waletao habari njema ya mambo mema, na wao waiambiao Sayuni: Tazama, Mungu wako anatawala! Kama dumande wa Karmeli, hivyo ndivyo maarifa juu ya Mungu yatakavyoshuka juu yao!

20 Na tena, tunasikia nini? Habari njema kutoka aKumora! bMoroni, malaika kutoka mbinguni, akitangaza utimilifu wa manabii—ckitabu kitafunuliwa. Sauti ya Bwana katika nyika za dFayette, wilaya ya Seneca, ikiwatangazia mashahidi watatu ekukishuhudia kitabu hicho! Sauti ya fMikaeli kando kando ya Susquehanna, akimfichua ibilisi wakati alipojitokeza kama malaika wa gnuru! Sauti ya hPetro, Yakobo, na Yohana nyikani kati ya Harmony, wilaya ya Susquehanna, na Colesville, wilaya ya Broome, kwenye mto Susquehanna waliposema wenyewe kuwa wanashikilia ifunguo za ufalme, na za kipindi cha utimilifu wa nyakati!

21 Na tena, sauti ya Mungu ndani ya chumba cha aBaba mzee Whitmer, huko Fayette, wilaya ya Seneca, na nyakati nyingine mbalimbali, na mahali mbali mbali wakati wa misafara yote na taabu za hili Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho! Na sauti ya Mikaeli, malaika mkuu, sauti ya bGabrieli, na ya cRafaeli, na dmalaika mbalimbali, kutoka Mikaeli au eAdamu kuja chini hadi wakati huu, wote wakitangaza fvipindi vyao, haki na utukufu wao, na nguvu za ukuhani wao; wakitoa mstari juu ya mstari, gkanuni juu ya kanuni; huku kidogo na kule kidogo; wakitupa faraja kwa kutangaza kile kitakachokuja, wakithibitisha hmatumaini yetu!

22 Ndugu, je, si lazima sisi tuendelee katika kazi hii iliyo kuu? Twende mbele na siyo nyuma. Tuweni wajasiri, ndugu; na mbele, mbele kwenye ushindi! Acheni mioyo yenu ifurahi, na kuwa na furaha kupita kiasi. Acheni nchi ipasuke kwa akuimba. Acheni wafu waimbe nyimbo za sifa ya milele kwa Mfalme bImanueli, aliyeagiza, kabla ya ulimwengu kuwepo, kile ambacho kingetuwezesha sisi ckuwakomboa kutoka dkifungoni mwao; kwani wafungwa watawekwa huru.

23 Acheni amilima ishangilie kwa shangwe, nanyi mabonde yote lieni kwa sauti; nanyi bahari zote na nchi kavu yatajeni maajabu ya Mfalme wenu wa Milele. Nanyi miito, chemichemi, na vijito, miminikeni kwa furaha. Acheni misitu na miti yote ya shamba imsifu Bwana; nanyi bmiamba lieni kwa shangwe! Na acheni jua, mwezi, na nyota za casubuhi ziimbe kwa pamoja, na watoto wote wa Mungu wapige kelele kwa shangwe! Acheni muumbaji wa milele atangaze jina lake milele na milele! Na tena ninasema, ni tukufu jinsi gani sauti tuisikiayo kutoka mbinguni, ikitangaza masikioni mwetu, utukufu, na wokovu, na heshima, na dmwili usiokufa, na euzima wa milele; falme, himaya, na nguvu.

24 Tazama, asiku iliyo kuu ya Bwana i karibu; na ni nani atakaye bstahimili siku ya kuja kwake, na ni nani atakayesimama wakati atakapoonekana? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu casafishaye, na mfano wa sabuni ya mtu afuaye; naye ataketi kama mtu dasafishaye fedha, naye atawasafisha wana wa eLawi, na atawasafisha kama dhahabu na fedha, ili wapate kutoa kwa Bwana fdhabihu katika haki. Kwa hiyo, sisi, kama kanisa na watu, na kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, tumtolee Bwana dhabihu katika haki; nasi tuonyeshe katika hekalu lake takatifu wakati litakapomalizika, kitabu chenye gkumbukumbu za wafu wetu, ambacho kitastahili kukubalika kote.

25 Ndugu zangu, ninayo mambo mengi ya kukuambieni juu ya jambo hili; lakini kwa sasa nitafunga, na kuendelea na jambo hili wakati mwingine. Mimi, daima, mtumishi wenu mnyenyekevu na rafiki asiye tetereka.

Joseph Smith.