Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 96


Sehemu ya 96

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii, ukionyesha mpangilio wa mji au kigingi cha Sayuni huko Kirtland, Ohio, 4 Juni 1833, kama mfano kwa Watakatifu hapo Kirtland. Tukio lilikuwa ni la mkutano wa makuhani wakuu, na ajenda kubwa ya kujadili ilikuwa ni ugawaji wa ardhi fulani, iliyojulikana kama shamba la French, lililokuwa likimilikiwa na Kanisa karibu na Kirtland. Kwa vile mkutano haukuweza kuafikiana nani alisimamie shamba hilo, wote walikubaliana kumwomba Bwana juu ya jambo hilo.

1, Kigingi cha Sayuni cha Kirtland kiimarishwe; 2–5, Askofu atagawa urithi huo kwa ajili ya Watakatifu; 6–9, John Johnson atakuwa mshiriki wa mpango wa ushirika.

1 Tazama, ninawaambia, hapa ndipo ilipo hekima, ambayo mtaweza kujua jinsi ya kutenda jambo hili, kwani ni muhimu kwangu kwamba akigingi hiki ambacho nimekiweka kuwa nguvu ya Sayuni chapaswa kuimarishwa.

2 Kwa hiyo, acha mtumishi wangu Newel K. Whitney asimamie mkuu wa mahali hapo palipotajwa miongoni mwenu, ambapo juu yake ninapanga kujenga nyumba yangu takatifu.

3 Na tena, pagawanywe katika viwanja, kulingana na hekima, kwa faida ya wale watafutao urithi, kama itakavyoamriwa katika baraza miongoni mwenu.

4 Kwa hiyo, hakikisheni mnalitazama jambo hili, na sehemu ile iliyo muhimu kwa manufaa ya aushirika wangu, kwa madhumuni ya kulileta neno langu kwa wanadamu.

5 Kwani tazama, amini ninawaambia, hili ni muhimu sana kwangu, kwamba neno langu lapaswa kuenea kwa wanadamu, kwa madhumuni ya kuilainisha mioyo ya wanadamu kwa faida yenu. Hivyo ndivyo. Amina.

6 Na tena, amini ninawaambia, ni hekima na ni muhimu kwangu, kwamba mtumishi wangu John Johnson ambaye matoleo yake nimeyakubali, na ambaye sala zake nimezisikia, ambaye kwake ninatoa ahadi ya uzima wa milele ilimradi kama atazishika amri zangu tokea sasa—

7 Kwani yeye ni mzaliwa wa ukoo wa aYusufu na mshirika wa baraka za ahadi zilizofanywa kwa baba zake—

8 Amini ninawaambia, ni muhimu kwangu kwamba awe mshiriki wa mpango wa ushirika, ili aweze kusaidia katika kulileta neno langu kwa wanadamu.

9 Kwa hiyo mtamtawaza katika baraka hii, naye lazima atafute kwa bidii yote kuyaondoa madeni yaliyopo juu ya nyumba iliyotajwa miongoni mwenu, ili aweze kuishi humo. Hivyo ndivyo. Amina.