Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 27


Sehemu ya 27

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith, Nabii, huko Harmony, Pennsylvania, Agosti 1830. Katika maandalizi ya ibada ambapo sakramenti ya mkate na divai ilikuwa itolewe, Joseph alikuwa akienda kununua divai. Alikutana na mjumbe kutoka mbinguni na akapokea ufunuo huu, ambao sehemu yake iliandikwa wakati huo, na iliyosalia iliandikwa mwezi uliofuata wa Septemba. Maji sasa yanatumika badala ya divai katika ibada ya sakramenti ya Kanisa.

1–4, Ishara zitakazotumika kupokea sakramenti zinaelezwa; 5–14, Kristo na watumishi Wake kutoka nyakati zote wanapokea Sakramenti; 15–18, Vaeni silaha za Mungu.

1 Sikilizeni sauti ya Yesu Kristo, Bwana wenu, Mungu wenu, na Mkombozi wenu, ambaye neno lake ni la aharaka na lenye nguvu.

2 Kwani, tazama, ninawaambia, kwamba si muhimu ni nini utakachokunywa au utakachokula wakati unapopokea asakramenti, ili mradi kwamba unafanya hayo kwa jicho likiwa kwenye butukufu wangu pekee—mkikumbuka kwa Baba mwili wangu uliotolewa kwa ajili yenu, na cdamu yangu iliyomwangwa kwa dondolea la dhambi zenu.

3 Kwa hiyo, amri ninakupa, kwamba usinunue divai wala kinywaji kikali cha adui zako;

4 Kwa hiyo, msipokee chochote isipokuwa kimetengenezwa upya miongoni mwenu; ndiyo, katika huu ufalme wa Baba yangu ambao utajengwa hapa duniani.

5 Tazama, hii ni hekima kwangu; kwa hiyo, usistaajabie, kwani saa yaja ambayo anitakunywa matunda ya mvinyo pamoja nanyi duniani, na pamoja na bMoroni, ambaye nilimtuma kwako kufichua Kitabu cha Mormoni, chenye utimilifu wa injili yangu isiyo na mwisho, ambaye nimemkabidhi funguo za kumbukumbu ya cfimbo ya Efraimu;

6 Na pia aElia, ambaye nimemkabidhi funguo za kukamilisha urejesho wa mambo yote yaliyonenwa kwa vinywa vya manabii watakatifu tangu mwanzo wa ulimwengu, kuhusu siku za mwisho;

7 Na pia Yohana mwana wa Zakaria, Zakaria ambaye yeye a(Elia) alimtembelea na kumpa ahadi kwamba atapata mwana, na jina lake litakuwa bYohana, na yeye atakuwa amejazwa na roho ya Elia;

8 Yohana ambaye nimekwisha mtuma kwenu ninyi, watumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na Oliver Cowdery, kuwatawaza ninyi katika aukuhani wa kwanza ambao mmeupokea, ili kwamba muwe mmeitwa na bkutawazwa kama ilivyokuwa hata kama cHaruni.

9 Na pia aEliya, ambaye kwake nimemkabidhi funguo za uwezo wa bkuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na mioyo ya watoto kwa baba, ili kwamba dunia yote isiweze kupigwa kwa laana.

10 Na pia pamoja na Yusufu na Yakobo, na Isaka, na Ibrahimu, baba zako, ambao hao aahadi zinabakia;

11 Na pia Mikaeli, au aAdamu, baba wa wote, mtawala wa wote, mzee wa siku;

12 Na pia pamoja na Petro, na Yakobo, na Yohana, ambao niliwatuma kwako, kwa wao animekutawazeni ninyi na kuwathibitisha kuwa bmitume, na cmashahidi maalumu wa jina langu, na kuchukua funguo za huduma yenu, na mambo yale yale niliyowafunulia wao;

13 Kwako wewe animekukabidhi bfunguo za ufalme wangu, na ckipindi cha dinjili kwa enyakati za mwisho; na kwa futimilifu wa nyakati, ambao ndani yake nitayakusanya gpamoja mambo yote, yaliyoko mbinguni na yaliyoko duniani;

14 Na pia wale wote ambao Baba yangu aamenipa mimi nje ya ulimwengu.

15 Kwa hiyo, inua moyo wako na ufurahie, na funga viuno vyako, na jitwalie aderaya zangu zote, upate kushindana siku ya uovu, na ukiisha kuyatimiza yote, uweze bkusimama.

16 Kwa hiyo, simama, ukiwa aumejifunga na bukweli kiunoni, na kuvaa cdirii ya dhaki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa injili ya eamani, ambayo nimemtuma fmalaika wangu kuikabidhi kwako;

17 Mkitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye amoto ya adui;

18 Na chukueni helmeti ya wokovu, na upanga wa Roho yangu, ambayo nitaimwaga juu yenu, na neno langu ambalo ninalifunua kwenu, na mpatane kuhusiana na jambo lolote mtakaloniomba Mimi, na kuweni waaminifu mpaka nijapo Mimi, na ninyi amtanyakuliwa, ili nilipo Mimi nanyi muwepo bpia. Amina.