Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 137


Sehemu ya 137

Ono lililotolewa kwa Joseph Smith Nabii, ndani ya hekalu huko Kirtland, Ohio, 21 Januari 1836. Tukio lilikuwa la huduma za ibada katika maandalizi kwa ajili ya uwekaji wakfu wa hekalu.

1–6, Nabii anamwona kaka yake Alvin katika ufalme wa selestia; 7–9, Mafundisho ya wokovu kwa ajili ya wafu yanafunuliwa; 10, Watoto wote wameokolewa katika ufalme wa selestia.

1 aMbingu zikatufunukia, nami nikauona ufalme wa bselestia wa Mungu, na utukufu wake, kama nilikuwa katika cmwili au nilikuwa nje ya mwili sijui.

2 Niliona uzuri uliopita kiasi wa alango ambalo warithi wa ufalme ule wataingia, ambalo lilikuwa mfano wa bmiale ya moto yenye kuzunguka;

3 Pia kiti cha enzi cha Mungu chenye akuwaka, juu yake bBaba na cMwana wamekaa.

4 Niliona mitaa mizuri ya ufalme ule, ambayo ilionekana kuwa kama umesakafiwa kwa adhahabu.

5 Nilimwona Baba aAdamu na bIbrahimu; na cbaba na dmama yangu; kaka yangu eAlvin, ambaye alifariki muda mrefu uliopita.

6 Na nikastaajabu jinsi gani ameweza kupata aurithi katika ufalme ule, nilitazama kwamba ameondoka katika maisha haya kabla Bwana hajaweka mkono wake kuwakusanya Israeli mara ya bpili, na wala chakubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi.

7 Na hivyo asauti ya Bwana ikanijia ikisema: Wote waliokufa bbila kuifahamu injili hii, ambao wangeliipokea kama wangeruhusiwa kuishi, watakuwa cwarithi wa ufalme wa dselestia wa Mungu;

8 Pia wale wote watakaokufa sasa na kuendelea bila kuifahamu, ambao awangeliipokea kwa moyo wao wote, watakuwa warithi wa ufalme huo;

9 Kwani Mimi, Bwana, anitawahukumu watu wote kulingana na bmatendo yao, kulingana na ctamaa za mioyo yao.

10 Nami pia niliona kwamba watoto wote ambao hufa kabla ya kufikia amiaka ya uwajibikaji bwanaokolewa katika ufalme wa selestia wa mbinguni.