Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 36


Sehemu ya 36

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Edward Partridge, huko karibu na Fayette, New York 9 Desemba 1830. (ona kichwa cha habari cha sehemu ya 35). Historia ya Joseph Smith inasema kwamba Edward Partridge “alikuwa mfano wa uchaji na mmoja wa watu wakuu wa Bwana.”

1–3, Bwana aweka mkono Wake juu ya Edward Partridge kwa mkono wa Sidney Rigdon; 4–8, Kila mwanaume aipokeaye injili na ukuhani aitwe kwenda kuihubiri.

1 Hivyo ndivyo asemavyo Bwana Mungu, aMwenye Enzi wa Israeli: Tazama, ninakuambia, mtumishi wangu bEdward, kwamba umebarikiwa, na dhambi zako zimesamehewa, na umeitwa ili kuitangaza injili yangu kama vile kwa sauti ya parapanda;

2 Na nitaweka amkono wangu juu yako kwa mkono wa mtumishi wangu Sidney Rigdon, nawe utampokea Roho wangu, Roho Mtakatifu, hata bMfariji, ambaye atakufundisha mambo ya camani yaliyo ya ufalme;

3 Nawe utatangaza kwa sauti kubwa, ukisema: Hosana, na libarikiwe jina la Mungu Aliye Juu Sana.

4 Na sasa wito huu na amri hii ninakupa wewe kuhusu watu wote—

5 Kwamba wale wote wajao mbele ya watumishi wangu Sidney Rigdon na Joseph Smith, Mdogo, wakiukumbatia wito huu na amri hizi, awatatawazwa na bkutumwa kuihubiri injili isiyo na mwisho miongoni mwa mataifa—

6 Tangazeni toba, mkisema: aJiokoeni wenyewe na kizazi hiki chenye ukaidi, na jitoeni huko kwenye moto, mkilichukia hata bvazi lililotiwa uchafu na mwili.

7 Na amri hii itatolewa kwa wazee wa kanisa langu, kwamba kila mtu ambaye ataikumbatia kwa moyo mmoja aweza kutawazwa na kutumwa, kama vile nilivyosema.

8 Mimi ndimi Yesu Kristo, Mwana wa Mungu; hivyo basi, funga viuno vyako na haraka naja kwenye ahekalu langu. Hivyo ndivyo. Amina.