Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 118


Sehemu ya 118

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Far West, Missouri, 8 Julai 1838, kama jibu la ombi, “Tuonyeshe mapenzi yako, Ee Bwana, juu ya Kumi na Wawili.”

1–3, Bwana atatoa mahitaji ya familia za Kumi na Wawili; 4–6, Nafasi katika Kumi na Wawili zinajazwa.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana: Acha mkutano ufanyike haraka; acha Kumi na Wawili wapangwe; na acha watu wateuliwe akujaza nafasi za wale walioanguka.

2 Acha mtumishi wangu aThomas abakie kwa kipindi kifupi katika nchi ya Sayuni, ili kuchapisha neno langu.

3 Acha waliosalia waendelee kuhubiri kutoka sasa, na kama watafanya hivi kwa unyenyekevu wote wa moyo, kwa upole na asubira, na buvumilivu, Mimi, Bwana, ninatoa kwao ahadi ya kuwa nitazitunza familia zao; na mlango wenye kuleta matokeo yanayotakiwa utafunguliwa kwa ajili yao, tangu sasa.

4 Na majira ya kuchipua yajayo acha waondoke kwenda kuvuka maji mengi, na huko wakatangaze injili yangu, utimilifu wake, na kulishuhudia jina langu.

5 Acha waondoke kutoka kwa watakatifu wangu katika mji wa Far West, siku ya tarehe ishirini na sita ya Aprili ijayo, kutoka mahali pa kiwanja cha kujenga nyumba yangu, asema Bwana.

6 Acha mtumishi wangu John Taylor, na pia mtumishi wangu John E. Page, na pia mtumishi wangu Wilford Woodruff, na pia mtumishi wangu Willard Richards, wateuliwe kujaza nafasi za wale ambao wameanguka, na waarifiwe rasmi juu ya uteuzi wao.