Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 26


Sehemu ya 26

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii, Oliver Cowdery, na John Whitmer, huko Harmony, Pennsylvania, Julai 1830 (ona kichwa cha habari cha sehemu ya 24).

1, Wameelekezwa kujifunza maandiko na kuhubiri; 2, Sheria ya maoni ya wengi yathibitishwa.

1 Tazama, ninawaambia kwamba muda wenu na utumike kwa kujifunza maandiko, na kuhubiri, na kwa kuthibitisha kanisa huko Colesville, na kufanya kazi zenu katika nchi, kama vile inavyotakiwa, hadi baada ya kwenda kule magharibi kufanya mkutano ujao; na ndipo itakapojulikana nini mtakachofanya.

2 Na mambo yote yafanyike kwa kauli ya pamoja katika kanisa, kwa sala nyingi na imani, kwani mambo yote mtayapokea kwa imani. Amina.