Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 53


Sehemu ya 53

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Algernon Sidney Gilbert, huko Kirtland, Ohio, 8 Juni 1831. Kwa maombi ya Sidney Gilbert, Nabii alimwuliza Bwana juu ya kazi na wito wa Ndugu Gilbert katika Kanisa.

1–3, Wito na uteule wa Sidney Gilbert katika Kanisa ni kutawazwa kuwa mzee; 4–7, Yeye pia atatumikia kama wakala wa askofu.

1 Tazama, ninakuambia, mtumishi wangu Sidney Gilbert, kwamba nimesikia sala zako; na umenilingana ili ijulikane kwako, na Bwana Mungu wako, juu ya wito na auteule wako katika kanisa, ambalo Mimi, Bwana nimelianzisha siku hizi za mwisho.

2 Tazama, Mimi, Bwana, ambaye anilisulubiwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, ninakupa amri kwamba yakupasa bkuachana na ulimwengu.

3 Jichukulie juu yako utawazo wangu, hata wa uzee wa Kanisa, kuhubiri imani na toba na aondoleo la dhambi, kulingana na neno langu, na kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa bmikono;

4 Na pia kuwa awakala kwa kanisa hili katika mahali ambapo utapangiwa na askofu, kulingana na amri ambazo zitatolewa hapo baadaye.

5 Na tena, amini ninakuambia, utafanya safari pamoja na watumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na Sidney Rigdon.

6 Tazama, hizi ni ibada za kwanza ambazo utazipokea; na mabaki yatajulikana wakati ujao, kulingana na utendaji kazi wako katika shamba la mizabibu.

7 Na tena, nataka ujifunze kwamba anaokolewa yule tu aastahimiliye hadi mwisho. Hivyo ndivyo. Amina.