Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 112


Sehemu ya 112

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Thomas B. Marsh, huko Kirtland, Ohio, 23 Julai 1837. Ufunuo huu unalo neno la Bwana kwa Thomas B. Marsh juu ya Mitume Kumi na Wawili wa Mwanakondoo. Ufunuo huu ulipokelewa siku ile Wazee Heber C. Kimball na Orson Hyde walipohubiri injili kwa mara ya kwanza huko Uingereza. Thomas B. Marsh kwa wakati huu alikuwa Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

1–10, Mitume Kumi na Wawili wataipeleka injili na kupaza sauti ya onyo kwa mataifa yote na watu wote; 11–15, Wao wataubeba msalaba wao, kumfuata Yesu, na kulisha kondoo Wake; 16–20, Wale waupokeao Urais wa Kwanza wampokea Bwana; 21–29, Giza limeifunika dunia, na ni wale tu waaminio na kubatizwa wataokolewa; 30–34, Urais wa kwanza na Mitume Kumi na Wawili wanashikilia funguo za kipindi cha utimilifu.

1 Amini hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwako wewe mtumishi wangu Thomas: Nimesikia sala zako; na sadaka zako zimefika juu kama aukumbusho mbele zangu, kwa niaba ya wale, ndugu zako, ambao walichaguliwa kutoa ushuhuda wa jina langu na bkuupeleka ulimwenguni kote miongoni mwa mataifa yote, makabila, lugha, na watu, na kutawazwa kwa njia ya watumishi wangu.

2 Amini ninakuambia, pamekuwepo na baadhi ya mambo machache moyoni mwako na pamoja nawe ambayo Mimi, Bwana, sikupendezwa nayo.

3 Hata hivyo, kwa vile wewe aumejidhili mwenyewe nawe utakwezwa; kwa hiyo, dhambi zako zote zimesamehewa.

4 Acha moyo wako na aufurahi mbele ya uso wangu; nawe utalishuhudia jina langu, siyo tu kwa bWayunani, bali pia kwa cWayahudi; nawe utalipeleka neno langu hata miisho ya dunia.

5 aJitahidi, kwa hiyo, asubuhi hadi asubuhi; na siku hadi siku na acha sauti yako ya bkuonya isikike; na usiku uingiapo usiache wakazi wa dunia walale, kwa sababu ya maneno yako.

6 Acha makazi yako yafahamike katika Sayuni, na ausiiondoe nyumba yako; kwa kuwa Mimi, Bwana, ninayo kazi kubwa ya kufanywa na wewe, kazi ya kulitangaza jina langu miongoni mwa wanadamu.

7 Kwa hiyo, afunga viuno vyako kwa ajili ya kazi hii. Na acha miguu yako ifungiwe pia, kwani wewe umechaguliwa, na njia zako zitakuwa miongoni mwa milima, na miongoni mwa mataifa mengi.

8 Na kwa neno lako wengi walio juu awatashushwa chini, na kwa neno lako wengi walio chini watakwezwa.

9 Acha sauti yako iwe karipio kwa wavunja sheria; na kwa kukaripia kwako ulimi wa mzushi na ukome uovu wake.

10 aJinyenyekeze; na Bwana Mungu wako atakuongoza kwa mkono, na kukupa jibu la sala zako.

11 Mimi naujua moyo wako, na nimesikia sala zako juu ya ndugu zako. Usiwe na aupendo zaidi kwao kuliko watu wengine wengi, bali acha upendo wako kwao uwe kama ujipendavyo wewe mwenyewe; na acha upendo wako ubaki kwa watu wote, na kwa wote walipendao jina langu.

12 Na uwaombee ndugu zako Kumi na Wawili. Waonye kwa nguvu kwa ajili ya jina langu, na acha waonywe kwa ajili ya dhambi zao zote, na uwe mwaminifu mbele zangu kwa ajina langu.

13 Na baada ya amajaribu yao, na btaabu nyingi, tazama, Mimi, Bwana, nitawatafuta, na kama hawakuishupaza mioyo yao, na kuzikaza shingo zao dhidi yangu, cwataongolewa, nami nitawaponya.

14 Sasa, ninakuambia, na hilo nikuambialo, nawaambia wote Kumi na Wawili: Inukeni na vifungeni viuno vyenu, chukua amsalaba wako, ukanifuate, na bkuwalisha kondoo zangu.

15 Msijikweze wenyewe; amsimuasi mtumishi wangu Joseph; kwani amini ninawaambia, Mimi nipo pamoja naye, na mkono wangu utakuwa juu yake; na bfunguo nilizompa yeye, na pia ninyi, hazitachukuliwa kutoka kwake hadi nitakapokuja.

16 Amini ninakuambia, mtumishi wangu Thomas, wewe ni mtu ambaye nimekuchagua kuzishika funguo za ufalme wangu, zinazowahusu Kumi na Wawili, popote miongoni mwa mataifa yote—

17 Ili upate kuwa mtumishi wangu kwa kufungua mlango wa ufalme mahali pote ambapo mtumishi wangu Joseph, na mtumishi wangu aSidney, na mtumishi wangu bHyrum, hawawezi kufika.

18 Kwani juu yao nimeweka mzigo wa makanisa yote kwa kipindi kifupi.

19 Kwa sababu hiyo, kokote watakakowatuma, nendeni, nami nitakuwa pamoja nanyi; na mahali popote mtakapotangaza jina langu mlango wa matokeo ya akufaa utafunguliwa kwenu, ili wapate kulipokea neno langu.

20 Yeyote aalipokeaye neno langu anipokea Mimi, na yeyote anipokeaye Mimi, huwapokea wale, Urais wa Kwanza, ambao nimewatuma, ambao nimewafanya kuwa washauri kwa ajili ya jina langu kwenu.

21 Na tena, ninawaambia, kwamba yeyote mtakayemtuma katika jina langu, kwa sauti ya ndugu zenu, hawa aKumi na Wawili, akiwa amependekezwa na kupewa bmamlaka kisheria na ninyi, atakuwa na uwezo wa kufungua mlango wa ufalme wangu kwa taifa lolote ambako ninyi mtawatuma—

22 Ilimradi kama watajinyenyekeza wenyewe mbele zangu, na kukaa katika neno langu, na akuisikia sauti ya Roho wangu.

23 Amini, amini, ninawaambia, agiza hufunika dunia, na giza kuu huzifunika akili za watu, na wenye mwili wote bwameharibika mbele za uso wangu.

24 Tazama, akisasi chaja haraka juu ya wakazi wa dunia, siku ya ghadhabu, siku ya kuteketezwa kwa moto, siku ya ukiwa, ya bkulia, ya kilio, na ya maombolezo; na kama tufani itakuja juu ya uso wote wa dunia, asema Bwana.

25 Na juu ya nyumba yangu aitaanzia, na kutoka nyumbani mwangu itaenea, asema Bwana;

26 Kwanza miongoni mwa wale walio miongoni mwenu, asema Bwana, ambao awamedai kulijua jina langu na bhawakunijua Mimi, nao cwamenitukana katikati ya nyumba yangu, asema Bwana.

27 Kwa hiyo, angalieni msijisumbue kuhusu mambo ya kanisa langu mahali hapa, asema Bwana.

28 Bali aitakaseni mioyo yenu mbele zangu, na ndipo bmwende ulimwenguni kote, na kuihubiri injili yangu kwa kila kiumbe ambacho bado hakijaipokea;

29 Na yule aaaminiye na bkubatizwa ataokolewa, na yule asiyeamini, na hakubatizwa, catalaaniwa.

30 Kwani kwenu, aKumi na Wawili, na wale, bUrais wa Kwanza wa Kwanza, ambao wameteuliwa na ninyi kuwa washauri wenu na viongozi wenu, ndiyo uwezo huu wa ukuhani umetolewa, kwa ajili ya siku za mwisho na kwa mara ya mwisho, ambacho ndicho ckipindi cha utimilifu wa nyakati.

31 Uwezo ambao ninyi mnaushikilia, kwa pamoja na wale wote waliopokea kipindi kwa wakati wowote kutoka mwanzo wa uumbaji;

32 Kwani amini ninawaambia, afunguo za kipindi, ambazo ninyi mmezipokea, bzimekuja chini kutoka kwa mababu, na mwisho wa yote, zimeshushwa kwenu kutoka mbinguni.

33 Amini ninawaambia, tazama wito wenu ni mkubwa kiasi gani. aIsafisheni mioyo yenu na mavazi yenu, isije damu ya kizazi hiki bikadaiwa mikononi mwenu.

34 Kuweni waaminifu hadi nijapo, kwani anaja upesi; na ujira wangu u pamoja nami kumlipa kila mtu kulingana na bkazi yake itakavyokuwa. Mimi ni Alfa na Omega. Amina.