Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 125


Sehemu ya 125

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Nauvoo, Illinois, Machi 1841, juu ya Watakatifu katika eneo la Iowa.

1–4, Watakatifu lazima waijenge miji na kukusanyika kwenye vigingi vya Sayuni.

1 Mapenzi ya Bwana ni yapi juu ya Watakatifu katika eneo la Iowa?

2 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, ninawaambia, kama wale awajiitao wenyewe kwa jina langu na wanajitahidi kuwa watakatifu wangu, kama watafanya mapenzi yangu na kushika amri zangu juu yao, acheni wajikusanye pamoja mahali ambapo nitawachagulia kwa njia ya mtumishi wangu Joseph, na waijenge miji kwa jina langu, ili wapate kuandaliwa kwa ajili ya kile kilicho wekwa kwa ajili ya wakati ujao.

3 Acheni waujenge mji kwa ajili ya jina langu juu ya ardhi iliyoko upande wa pili wa mji wa Nauvoo, na acheni jina la aZarahemla liitwe juu yake.

4 Na acheni wale wote wanaokuja kutoka mashariki, na magharibi, na kaskazini, na kusini, ambao wanataka kuishi humo, wachukue urithi wao humo humo, na pia katika mji wa aNashville, au katika mji wa Nauvoo, na katika bvigingi vyote nilivyoviteua, asema Bwana.