Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 70


Sehemu ya 70

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Hiram, Ohio, 12 Novemba 1831. Historia ya Nabii inaeleza kuwa mikutano minne maalumu ilikuwa imefanyika kutoka tarehe 1 hadi 12 ya Novemba, kwa pamoja. Katika mkutano wa mwisho kati ya mikutano hii, umuhimu mkubwa wa mafunuo ambayo baadae yangekuja kuchapishwa kama Book of Commandments (Kitabu cha Amri) na baadaye Mafundisho na Maagano, ulifikiriwa. Ufunuo huu ulitolewa baada ya mkutano kupiga kura kwamba mafunuo yalikuwa “ya thamani kwa Kanisa kuliko utajiri wote wa Dunia.” Historia ya Joseph Smith inayataja mafunuo haya kuwa ni “msingi wa Kanisa katika siku hizi za mwisho, na ni ya manufaa kwa ulimwengu, yakionyesha kwamba funguo za siri za ufalme wa Mwokozi wetu zimekabidhiwa tena kwa mwanadamu.”

1–5, Wasimamizi wanateuliwa kuchapisha mafunuo; 6–13, Wale watendao kazi katika mambo ya kiroho wanastahili ujira wao; 14–18, Watakatifu wanapaswa kuwa sawa katika mambo ya kimwili.

1 Tazama, na sikilizeni, Enyi wakazi wa Sayuni, na watu wote wa kanisa langu mlio mbali, na sikilizeni neno la Bwana ambalo ninalitoa kwa mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na pia kwa mtumishi wangu Martin Harris, na pia kwa mtumishi wangu Oliver Cowdery, na pia kwa mtumishi wangu John Whitmer, na pia kwa mtumishi wangu Sidney Rigdon, na pia kwa mtumishi wangu William W. Phelps, kama amri kwao.

2 Kwani ninatoa kwao amri; kwa hivyo sikilizeni na msikie, kwani hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwao—

3 Mimi, Bwana, nimewateua, na kuwatawaza kuwa awasimamizi wa mafunuo na amri ambazo nimezitoa kwao, na zile ambazo nitazitoa kwao hapo baadaye;

4 Na taarifa ya usimamizi huu nitawadai hao katika siku ya hukumu.

5 Kwa hiyo, mimi nimeikabidhi kwao, na hii ni kazi yao katika kanisa la Mungu, kusimamia na mambo yahusikanayo, ndiyo, na manufaa yake.

6 Kwa hiyo, amri ninaitoa kwao, kwamba hawatayatoa mambo haya kwa kanisa, wala kwa walimwengu;

7 Hata hivyo, kadiri watakavyopokea zaidi ya mahitaji kwa mahitaji yao ya lazima na yasiyo ya lazima, wayapeleke katika aghala yangu;

8 Na manufaa hayo yawekwe wakfu kwa ajili ya wakazi wa Sayuni, na kwa vizazi vyao, ilimradi wamekuwa awarithi kulingana na sheria za ufalme.

9 Tazama, hili ndilo alitakalo Bwana kwa kila mtu katika ausimamizi wake, hata kama vile Mimi, Bwana, nilivyoteua au nitakavyoteua hapo baadaye kwa kila mtu.

10 Na tazama, hakuna aliyesamehewa kutoka sheria hii aliye wa kanisa la Mungu aliye hai;

11 Ndiyo, si askofu, wala awakala ambaye atunzaye ghala ya Bwana, wala yule aliyeteuliwa katika usimamizi juu ya mambo ya kimwili.

12 Yule aliyeteuliwa kusimamia katika mambo ya kiroho, naye aanastahili ujira wake, kama vile wale walioteuliwa katika usimamizi wa kuhudumu katika mambo ya kimwili;

13 Ndiyo, hata kwa wingi sana, wingi ambao huzidishwa kwao kwa njia ya mafunuo ya Roho.

14 Hata hivyo, katika mambo ya kimwili mtakuwa asawa, na hii isiwe kwa kinyongo, vinginevyo uwingi wa mafunuo ya Roho yatazuiliwa.

15 Sasa, aamri hii nimetoa kwa watumishi wangu kwa faida yao wakati wangali hai, kama ishara ya baraka zangu juu ya vichwa vyao, na kama thawabu ya bbidii yao na kwa usalama wao;

16 Kwa chakula na kwa amavazi; kwa urithi; kwa nyumba na kwa ardhi, katika hali yoyote Mimi, Bwana, nitakayowaweka, na mahali popote ambapo Mimi, Bwana, nitawatuma.

17 Kwani wamekuwa waaminifu juu ya amambo mengi, na wamefanya vizuri mradi tu hawakutenda dhambi.

18 Tazama, Mimi, Bwana ni mwenye ahuruma na nitawabariki, na wataingia katika shangwe ya mambo haya. Hivyo ndivyo. Amina.