Maandiko
1 Nefi 8
iliyopita inayofuata

Mlango wa 8

Lehi anaona ono la mti wa uhai—Anakula matunda yake na kutamani jamii yake pia nao wale—Anaona fimbo ya chuma, na njia nyembamba imesonga, na ukungu wa giza ambao unafunika wanadamu—Saria, Nefi, na Samu wanakula matunda, lakini Lamani na Lemueli wanakataa. Karibia mwaka 600–592 K.K.

1 Na ikawa kwamba tulikuwa tumekusanya namna zote za mbegu za kila aina, pamoja na nafaka za kila aina, na pia mbegu za kila aina ya matunda.

2 Na ikawa kwamba wakati baba yangu alipoishi nyikani alituzungumzia, akisema: Tazama, animeota ndoto; au kwa maneno mengine, nimeona bono.

3 Na tazama, kwa sababu ya kitu ambacho nilikuwa nimekiona, nina sababu ya kutoa shukrani kwa Bwana kwa sababu ya aNefi na pia ya Samu; nina sababu ya kuamini kwamba wao, na pia wengi wa uzao wao, watakombolewa.

4 Lakini tazama, aLamani na Lemueli, ninaogopa sana kwa sababu yenu; kwani tazama, nilidhania niliona ndotoni mwangu, nyika yenye giza na yenye kuhuzunisha.

5 Na ikawa kwamba niliona mtu, na alikuwa amevaa ajoho jeupe; na akaja na kusimama mbele yangu.

6 Na ikawa kwamba alinizungumzia, na aliniamuru nimfuate.

7 Na ikawa kwamba nilipokuwa namfuata nilijiona kwamba nilikuwa katika mahali penye giza na ukiwa wa jangwa.

8 Na baada ya kusafiri kwa masaa mengi gizani, nilianza kumwomba Bwana aanihurumie, kulingana na wingi wa rehema na fadhili zake.

9 Na ikawa kwamba baada ya mimi kumwomba Bwana, niliona auwanja mkubwa na mpana.

10 Na ikawa kwamba niliona amti, ambao bmatunda yake yalitamanika kumfurahisha mwanadamu.

11 Na ikawa kwamba nilienda na nikala amatunda yake; na nikagundua kwamba yalikuwa matamu, zaidi ya yote ambayo nilikuwa nimeonja. Ndiyo, na nikaona kwamba tunda lake lilikuwa leupe, kushinda bweupe wote ambao nilikuwa nimeuona.

12 Na nilipokula tunda lile lilijaza nafsi yangu na ashangwe tele; kwa hivyo, nikaanza bkutaka jamii yangu na wao pia wale; kwani nilijua kwamba lilikuwa tunda la ckupendeza zaidi ya yote.

13 Na nilipotazama hapa na pale, ili pia labda nione jamii yangu, niliona amto wa maji; na ulitiririka, karibu na mti ule ambao nilikuwa nikila matunda yake.

14 Na nikatazama nione ulitoka wapi; na nikaona chimbuko lake mbali kidogo; na kwenye chimbuko nikaona mama yenu Saria, na Samu, na Nefi; na walisimama wakawa kama hawajui wanapoenda.

15 Na ikawa kwamba niliwapungia mkono; na pia kwa sauti kubwa nikawaambia wanikaribie, na wale tunda, ambalo lilikuwa la kupendeza zaidi kuliko tunda lingine.

16 Na ikawa kwamba walinikaribia na kula tunda pia.

17 Na ikawa kwamba nilitaka pia Lamani na Lemueli waje na kula tunda; kwa hivyo, nikatazama kwenye chimbuko la mto, kwamba labda niwaone.

18 Na ikawa kwamba niliwaona, lakini ahawakunijia na kula tunda.

19 Na nikaona afimbo ya chuma, na ilinyooka kando ya ukingo wa mto, mpaka kwenye mti niliposimama.

20 Na pia nikaona njia nyembamba aimesonga, ambayo iliambatana na fimbo ya chuma, hata hadi ambapo nilipokuwa nimesimama kwenye mti; na pia ilielekea kwenye chimbuko la chemchemi, hadi kwenye buwanja mkubwa mpana, kama kwamba ni ulimwengu.

21 Na nikaona umati mkubwa wa watu usio na idadi, wengi wao ambao walikuwa wanasogea mbele, ili wapate kufikia anjia ambayo ilielekea kwenye mti ambapo nilikuwa nimesimama.

22 Na ikawa kwamba walifika hapo mbele, na kuipata njia iliyoelekea kwenye mti.

23 Na ikawa kwamba kulitokea aukungu wa giza; ndiyo, hata ukungu mkubwa wa giza, hadi wale ambao walikuwa wametangulia njia walipotea njia, kwamba walizungukazunguka na kupotea.

24 Na ikawa kwamba niliona wengine wakisonga mbele, na wakafika mbele na wakashika mwisho wa fimbo ya chuma; na wakasonga mbele na kupenya ukungu wa giza, wakishikilia fimbo ya chuma, hadi wakafika na kula amatunda ya mti.

25 Na baada ya kula matunda ya mti wakatupa macho yao hapa na pale wakawa kama awanaaibika.

26 Na pia nikatupa macho yangu hapa na pale, na nikaona, kwenye ngʼambo nyingine ya mto wa maji, jengo kubwa na apana; na lilikuwa ni kama linaelea hewani, juu zaidi ya ardhi.

27 Na lilikuwa limejaa watu, wazee kwa vijana, wanaume kwa wanawake; na mavazi yao yalikuwa mazuri kupita kiasi; na walikuwa na atabia ya kufanya mzaha na kuwaonyesha kwa vidole vyao wale ambao walikuwa wanakuja na kula matunda.

28 Na baada ya akuonja matunda bwaliaibika, kwa sababu ya wale waliokuwa wakiwadharau; na cwakaingia katika njia zilizokataliwa na wakapotea.

29 Na sasa mimi, Nefi, sizungumzi maneno ayote ya baba yangu.

30 Lakini, nikifupisha katika kuandika, tazama, aliona umati mwingine ukisonga mbele; na wakaja na kushika mwisho wa ile fimbo ya chuma; na wakasonga mbele, daima wameshikilia ile afimbo ya chuma, hadi wakafika na kuinama na kula matunda ya ule mti.

31 Na pia akaona aumati mwingine ukipapasapapasa wakielekea kwa lile jengo kubwa na pana.

32 Na ikawa kwamba wengi walizama kwenye kilindi cha achemchemi; na wengi wakapotea asipate kuwaona, wakizururazurura katika njia ngeni.

33 Na umati ule ulioingia kwenye lile jengo geni ulikuwa mkubwa. Na baada ya kuingia kwenye lile jengo walitufanyia ishara za amadharau kwa vidole vyao mimi na wale ambao walikuwa wakila matunda; lakini hatukuwasikiza.

34 Haya ndiyo maneno ya baba yangu: Kuwa wengi awaliowasikiza, walianguka.

35 Na aLamani na Lemueli hawakula lile tunda, alisema baba yangu.

36 Na ikawa kwamba baada ya baba yangu kuzungumza maneno yote ya ndoto yake au ono, ambayo yalikuwa mengi, akatuambia sisi, kwa sababu ya vitu hivi vyote ambavyo alivyoona katika ono, aliwahofia kupita kiasi Lamani na Lemueli; ndiyo, alihofia wasije wakatupiliwa mbali kutoka kwenye uwepo wa Bwana.

37 Na aliwasihi kwa huruma zote za amzazi mwenye upendo, kwamba wasikilize maneno yake, na pengine Bwana angewarehemu, na asiwatupilie mbali; ndiyo, baba yangu aliwahubiria.

38 Na baada ya kuwahubiria, na pia kuwatolea unabii wa vitu vingi, aliwaamuru kuweka amri za Bwana; na akakoma kuwazungumzia.