Maandiko
1 Nefi 20
iliyopita inayofuata

Mlango wa 20

Bwana anafunua makusudi Yake kwa Israeli—Israeli imechaguliwa kutoka katika tanuri la masumbuko na linapaswa kuondoka kutoka Babeli—Linganisha Isaya 48. Karibia mwaka 588–570 K.K.

1 Sikilizeni na msikie haya, Ee nyumba ya Yakobo, ambao wanajulikana kwa jina la Israeli, na wametoka katika maji ya Yuda, au kutoka kwenye maji ya aubatizo, ambao wanaapa kwa jina la Bwana, na kutaja Mungu wa Israeli, walakini hawaapi kwa ukweli wala kwa haki.

2 Walakini, wanajiita wakaazi wa amji mtakatifu, lakini hawamtegemei Mungu wa Israeli, ambaye ni Bwana wa Majeshi; ndiyo, jina lake ni Bwana wa Majeshi.

3 Tazama, nimetangaza vitu vilivyokuja aawali kutoka mwanzoni; na yalitoka kinywani mwangu, na niliyadhihirisha. Niliyadhihirisha kwa ghafla.

4 Na niliitenda kwa sababu nilijua kwamba awewe ni mkaidi, na shingo yako ni ngumu kama chuma, na paji lako kama shaba nyeupe;

5 Na nimekutangazia hata tangu mwanzo, kabla hayajakuwa niliyaonyesha kwako; na nilikuonyesha usije ukasema—aSanamu yangu imezitenda, na mfano uliochongwa wangu, na mfano ulioyeyushwa wangu ndiyo imeziamuru.

6 Umeona na kusikia haya yote; na je wewe hutayatangaza? Na kwamba nimekuonyesha vitu vipya tangu wakati huu, hata vitu vilivyofichwa, na wewe hukuvijua.

7 Yameumbwa sasa, na si tangu mwanzo, hata kabla ya ile siku ambayo hukuyasikia yalikuwa yametangazwa kwako, ili usiseme—Tazama niliyajua.

8 Ndiyo, na wewe hukusikia; ndiyo, wewe hukujua; ndiyo, tangu ule wakati sikio lako halikufunguliwa; maana nilijua kwamba ungetenda uhaini, na ulikuwa amvunja sheria kutoka tumboni.

9 Walakini, kwa sababu ya heshima ya ajina langu nitazuia ghadhabu yangu, na kwa sababu ya sifa zangu nitajizuia kutokana nawe, kwamba nisikuangamize.

10 Kwani, tazama, nimekutakasa, nimekuchagua kutoka karibu ya amasumbuko.

11 Kwa heshima yangu, ndiyo, kwa heshima yangu nitatenda hii, kwani sitakubali ajina langu lichafuliwe, na bsitampatia mwingine utukufu wangu.

12 Nisikilize mimi, Ee Yakobo, na Israeli wateule wangu, kwani Mimi ndimi yeye; Mimi ndimi wa akwanza, na pia Mimi ndimi wa mwisho.

13 Mkono wangu pia aumejenga msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umetandaza mbingu. Naziita na zinasimama pamoja.

14 Ninyi nyote, kusanyikeni, na msikie; ni nani miongoni mwao amewatangazia vitu hivi? Bwana amempenda; ndiyo, na aatatimiza neno lake ambalo amesema kupitia kwao; na atatendea bBabilonia nia yake, na mkono wake utanyoshewa Wakaldayo.

15 Pia, Bwana asema; mimi, Bwana, ndiyo, nimesema; ndiyo, nimemuita kutangaza, nimemleta, na atafanikiwa katika njia zake.

16 Njooni karibu na mimi; sijazungumza kwa asiri; tangu mwanzo, tangu ilipotangazwa nimezungumza; na Bwana Mungu, na Roho yake, amenituma.

17 Na hivyo ndivyo asemavyo Bwana, aMkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli; nimemtuma, Bwana Mungu wenu anayekufundisha kufaidika, ambaye banakuongoza katika njia inayokupasa, ameitenda.

18 Ee kwamba ungesikiliza aamri zangu—basi amani yako ingekuwa kama mto, na haki yako ungekuwa kama mawimbi ya bahari.

19 aUzao wako ungekuwa pia kama mchanga; na kizazi cha matumbo yenu ingekuwa kama changarawe yake; jina lake halingetupiliwa mbali wala kuangamizwa kutoka mbele yangu.

20 aTokeni kutoka Babilonia, waondokeeni Wakaldayo, kwa sauti ya kuimba tangazeni ninyi, semeni haya, ambieni hadi mwisho wa ulimwengu; semeni ninyi; Bwana amemkomboa bmtumishi wake Yakobo.

21 Na hawakuona akiu; aliwaongoza katika majangwa; akasababisha maji kutiririka kutoka kwenye bmwamba kwa sababu yao; alipasua mwamba pia na maji yakatoka.

22 Ingawa ametenda haya yote, na makuu pia, hakuna aamani, asema Bwana, kwa waovu.