Maandiko
1 Nefi 18


Mlango wa 18

Merikebu inamalizika—Kuzaliwa kwa Yakobo na Yusufu kunatajwa—Kundi lapakia kuelekea nchi ya ahadi—Wana wa Ishmaeli na wake zao wanaungana kwa kuasi na ugomvi—Nefi anafungwa, na merikebu inarudishwa nyuma na dhoruba kubwa—Nefi anaachiliwa huru, na kwa sala zake dhoruba inatulia—Watu wanawasili katika nchi ya ahadi. Karibia mwaka 591–589 K.K.

1 Na ikawa kwamba walimuabudu Bwana, na wakajiunga na mimi; na tukaunda mbao kwa ufundi maalumu. Na Bwana alinionyesha mara kwa mara namna ya kuunda zile mbao za merikebu.

2 Sasa mimi, Nefi, sikuunda mbao kulingana na njia zilizofahamika kwa watu, wala sikujenga merikebu kulingana na njia za watu; lakini niliijenga kulingana na vile Bwana alivyonionyesha; kwa hivyo, haikuwa kulingana na njia za wanadamu.

3 Na mimi, Nefi, nilienda mlimani mara nyingi, na anilimuomba Bwana mara nyingi; kwa hivyo Bwana balinionyesha vitu vikubwa.

4 Na ikawa kwamba baada ya mimi kumaliza kujenga merikebu, kulingana na neno la Bwana, ndugu zangu waliona kwamba ni nzuri, na ufundi wake ulikuwa stadi; kwa hivyo, awakajinyenyekeza tena kwa Bwana.

5 Na ikawa kwamba sauti ya Bwana ikamjia baba yangu, kwamba tuinuke na kuingia kwenye merikebu.

6 Na ikawa kwamba kesho yake, baada ya kutayarisha vitu vyote, matunda mengi na anyama kutoka nyikani, na asali nyingi, na maakuli kulingana na yale Bwana aliyotuamuru, tuliingia kwenye merikebu, pamoja na mizigo yetu yote na mbegu zetu, na kitu chochote ambacho tulileta nasi, kila mmoja kulingana na umri wake; kwa hivyo, tuliingia sote kwenye merikebu, pamoja na wake zetu na watoto wetu.

7 Na sasa, baba yangu alikuwa amepata watoto wawili nyikani; mkubwa aliitwa aYakobo na mdogo alikuwa ni bYusufu.

8 Na ikawa kwamba baada ya sisi sote kuingia kwenye merikebu, na kuchukua maakuli yetu na vitu ambavyo tuliamriwa, tulitweka abaharini na tukaendeshwa mbele na upepo tukielekea bnchi ya ahadi.

9 Na baada ya sisi kuendeshwa na upepo kwa muda wa siku nyingi, tazama, kaka zangu na wana wa Ishmaeli pia na wake zao walianza kujifurahisha, hata wakaanza kucheza ngoma, na kuimba, na kuzungumza kwa ujeuri sana, ndiyo, hata kwamba wakasahau kwa nguvu gani waliletwa hapo; ndiyo, waliinuliwa zaidi kwa ujeuri.

10 Na mimi, Nefi, nikaanza kuogopa zaidi kwamba Bwana atatukasirikia, na atupige kwa sababu ya uovu wetu, hata tuzame kwenye kilindi cha bahari; kwa hivyo, mimi, Nefi, nilianza kuwazungumzia kwa makini; lakini tazama awalinikasirikia, wakisema: Hatutakubali kuwa mdogo wetu awe bmtawala wetu.

11 Na ikawa kwamba Lamani na Lemueli walinikamata na kunifunga kwa kamba, na wakawa wakali sana kwangu; walakini, Bwana aalikubali haya ili aonyeshe nguvu zake, kwa kutimiza maneno yake aliyosema kuhusu wale waovu.

12 Na ikawa kwamba waliponifunga hata nisingeweza kutembea, adira, ambayo Bwana alikuwa ameitayarisha, ilikoma kufanya kazi.

13 Kwa hivyo, hawakujua njia gani ambayo wangeelekeza merikebu, hata mpaka kukawa na dhoruba kubwa, ndiyo, dhoruba kuu na kali, na atukarudishwa nyuma majini kwa muda wa siku tatu; na wakaanza kuogopa kupita kiasi kwamba watazama baharini; walakini hawakunifungua.

14 Na baada ya kurudishwa nyuma kwa siku nne, dhoruba ilianza kuwa kali zaidi.

15 Na ikawa kwamba tulikuwa karibu kumezwa kilindini mwa bahari. Na baada ya kurudishwa nyuma katika maji kwa muda wa siku nne, kaka zangu wakaanza akuona kwamba hukumu za Mungu zilikuwa juu yao, na kwamba lazima wafe kama hawatatubu maovu yao; kwa hivyo, wakanijia na kunifungua kamba ambazo zilikuwa kwenye viwiko vyangu, na tazama vilikuwa vimefura zaidi; na pia vifundo vyangu vilivimba sana, na uchungu ulikuwa mwingi.

16 Walakini, nilimtazama Mungu wangu, na anilimsifu siku yote nzima; na sikumlalamikia Bwana kwa sababu ya masumbuko yangu.

17 Sasa baba yangu, Lehi, alikuwa amewaambia vitu vingi, na pia kwa wana wa aIshmaeli; lakini, tazama, walitoa vitisho vingi kwa yeyote ambaye alinitetea; na wazazi wangu wakiwa na umri mkuu, na wakiwa wameteseka kwa hofu kuu kwa sababu ya wana wao, walilemewa, ndiyo, hadi wakaugulia vitandani.

18 Kwa sababu ya hofu yao na huzuni nyingi, na maovu ya kaka zangu, walikaribia kukutana na Mungu wao; ndiyo, mvi zao zilikaribia kulazwa mavumbini; ndiyo, hata karibu watupwe na huzuni katika kaburi la maji.

19 Na Yakobo na Yusufu pia, wakiwa wachanga, na wakihitaji kulishwa sana, walihuzunishwa na masumbuko ya mama yao; pia na amke wangu na machozi yake na sala, na pia watoto wangu, hawakulainisha mioyo ya kaka zangu ili wanifungue.

20 Na hapakuwa chochote ila nguvu za Mungu, zilizowatisha na maangamizo, kingelainisha mioyo yao; kwa hivyo, walipoona kwamba walikuwa karibu kuzama baharini walitubu kwa kitu kile ambacho walitenda, hata wakanifungua.

21 Na ikawa kwamba baada ya wao kunifungua, tazama, nilichukua dira, na ilitenda nilivyotaka. Na ikawa kwamba nikamwomba Bwana; na baada ya mimi kusali, upepo ulikoma, na dhoruba ikaisha, na kukawa na utulivu mkuu.

22 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, niliendesha merikebu, hata tukasafiri tena tukielekea nchi ya ahadi.

23 Na ikawa kwamba baada ya kusafiri kwa muda wa siku nyingi tuliwasili katika anchi ya ahadi; na tukatembea kwenye ardhi, na tukapiga hema zetu; na tukaiita nchi ya ahadi.

24 Na ikawa kwamba tulianza kulima ardhi, na tukaanza kupanda mbegu; ndiyo, tulitia mbegu zetu zote udongoni, tulizokuwa tumebeba kutoka nchi ya Yerusalemu. Na ikawa kwamba zilimea zaidi; kwa hivyo, tukapata baraka tele.

25 Na ikawa kwamba tuliposafiri nyikani, tulipata katika nchi ya ahadi, wanyama huko porini wa kila aina, ngombe na dume, na punda na farasi, na mbuzi wa nyumbani na mbuzi wa kichaka, na kila aina ya wanyama wa mwitu, ambao walimfaidisha mwanadamu. Na tukapata kila aina ya mawe yenye madini, ya dhahabu, na ya fedha, na shaba nyekundu.