Maandiko Matakatifu
1 Nefi 21


Mlango wa 21

Masiya atakuwa nuru ya Wayunani na atawafungua wafungwa—Israeli itakusanywa kwa uwezo katika siku za mwisho—Wafalme watakuwa baba zao walezi—Linganisha Isaya 49. Karibia mwaka 588–570 K.K.

1 Na tena: Sikiliza, Ee ninyi nyumba ya Israeli, nyote ambao mmetenganishwa na kufukuzwa kwa sababu ya uovu wa wachungaji wa watu wangu; ndiyo, ninyi nyote ambao mmetenganishwa, na kutawanywa ugenini, wale ambao ni wa watu wangu, Ee nyumba ya Israeli. Sikilizeni, Ee avisiwa, nisikilizeni mimi, na watu walio bmbali pia sikilizeni; Bwana ameniita kabla sijazaliwa, kutoka tumboni mwa mama yangu, ametaja jina langu.

2 Na amefanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; amenificha katika kivuli cha mkono wake, na akanifanya mshale uliongʼaa; amenificha katika podo lake.

3 Na akaniambia: Wewe ndiye amtumishi wangu, Ee Israeli, ambaye nitatukuzwa ndani yake.

4 Kisha nikasema, nimefanya kazi bure, nimetumia nguvu zangu bure na bila faida; kwa hakika hukumu yangu iko na Bwana, na vitendo vyangu na Mungu wangu.

5 Na sasa, asema Bwana—ambaye aaliniumba kutoka tumboni ili niwe mtumishi wake, kumrejesha Yakobo kwake tena—ingawa Israeli haijakusanyika, bado nitakuwa mwenye utukufu machoni mwa Bwana, na Mungu wangu atakuwa nguvu yangu.

6 Na alisema: Ni kitu rahisi kuwa wewe uwe mtumishi wangu ili uinue amakabila ya Yakobo, na kurudisha waliohifadhiwa kutoka Israeli. Nitakufanya pia uwe bnuru kwa cWayunani, kwamba uwe wokovu wangu hadi mwisho wa ulimwengu.

7 Hivyo ndivyo asemavyo Bwana, Mkombozi wa Israeli, Mtakatifu wake, kwa yule anayechukiwa na watu, kwa yule anaye dharauliwa na mataifa, kwa mtumishi wa watawala: Wafalme wataona na kuinuka, wana wa wafalme pia wataabudu, kwa sababu ya Bwana ambaye ni mwaminifu.

8 Hivyo ndivyo asemavyo Bwana: Kwa wakati uliokubalika nimekusikia, Ee visiwa vya bahari, na kwa siku ya wokovu nilikusaidia; na nitakuhifadhi, na ninakupatia amtumishi wangu uwe agano la watu, kuimarisha nchi, kuwasababisha kurithi makao yaliokuwa yenye ukiwa.

9 Ili uwaambie awafungwa: Ondokeni; kwa wale ambao wanaketi bgizani: Jidhihirisheni. Watakula njiani, na cmalisho yao yatakuwa juu ya majabali.

10 Hawataona njaa wala kiu, wala joto au jua kuwachoma; kwani yule anayewarehemu atawaongoza, hata kwenye chemchemi za maji atawaongoza.

11 Na nitafanya milima yangu yote iwe anjia, na njia zangu zitainuliwa.

12 Na kisha, Ee nyumba ya Israeli, tazama, ahaya yatatoka mbali; na tazama, haya kutoka kaskazini na kutoka magharibi; na haya kutoka nchi ya Sinimu.

13 aImbeni, Ee mbingu; na ushangilie, Ee dunia; kwani miguu ya wale ambao wako mashariki itaimarishwa; na anzeni kuimba, Ee milima; kwani hawatapigwa tena; kwani Bwana amewafariji watu wake, na atawarehemu wanaosumbuka.

14 Lakini, tazama, Sayuni imesema: Bwana ameniacha, na Bwana wangu amenisahau—lakini ataonyesha kwamba hajafanya hivyo.

15 Kwani amwanamke anaweza kusahau mtoto wake ambaye anamnyonyesha, kwamba asiwe na huruma kwa mwana wa tumbo lake? Ndiyo, wanaweza bkusahau, lakini sitakusahau, Ee nyumba ya Israeli.

16 Tazama, nimekuchora aviganjani mwa mikono yangu; kuta zako daima ziko mbele yangu.

17 Watoto wako wataharakisha dhidi ya waharibifu wako; na wale awaliokuharibu wataondoka kutoka kwako.

18 Inua macho yako pande zote na utazame; hawa wote awanakusanyika pamoja, na watakuja kwako. Na vile ninavyoishi, Bwana asema, wewe utajivika na wao wote, kama pambo, na kujifunga kwao kama bibi arusi.

19 Kwani utupu wako na kwenye ukiwa, na nchi yako ya maangamizo, itakuwa hata sasa nyembamba kwa sababu ya wakazi; na wale ambao walikumeza watakuwa mbali.

20 Watoto utakaopata, baada ya kupoteza wale wa kwanza, watasema tena masikioni mwako: Hapa mahali ni apadogo sana kwangu; nipe mahali ili niishi.

21 Kisha autasema moyoni mwako: Nani alinizalia hawa, akiona nimepoteza watoto wangu, na nina bukiwa, mtumwa, na akizurura hapa na pale? Nani amelea hawa? Tazama, niliachwa pekee yangu; hawa, walikuwa wapi?

22 Hivyo ndivyo asemavyo Bwana Mungu: Tazama, nitawanyooshea aWayunani mkono wangu, na nitapeperusha bbendera yangu miongoni mwa watu; na wataleta wana wako kwa cmikono yao, na mabinti zako watabebwa mabegani mwao.

23 Na awafalme watakuwa baba zako walezi, nao malkia wao watakuwa mama zako bwalezi; watainama mbele yako nyuso zao zikiielekea ardhi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; na utajua kwamba mimi ni Bwana; kwani hawataaibika cwanaoningojea.

24 Kwani mateka watanyakuliwa kutoka kwa shupavu, au awatumwa halali kukombolewa?

25 Lakini hivyo ndivyo asemavyo Bwana, hata watumwa wa shupavu watachukuliwa, na mateka wa wale walio wa kutisha watakombolewa; kwani nitashindana na yule anayeshindana nawe, na nitaokoa watoto wako.

26 Na anitawalisha wanaokudhulumu kwa nyama yao wenyewe; watalewa kwa damu yao wenyewe kama kwa mvinyo mtamu; na watu wote bwatajua kwamba mimi, Bwana, ni Mwokozi wenu na Mkombozi wenu, cMwenyezi Mkuu wa Yakobo.