Maandiko Matakatifu
Mormoni 7


Mlango wa 7

Mormoni anawaalika Walamani wa siku za mwisho kuamini katika Kristo, waikubali injili Yake, na waokolewe—Wote wanaoiamini Biblia pia wataamini Kitabu cha Mormoni. Karibia mwaka 385 B.K.

1 Na sasa, tazama, nataka kuzungumza machache kwa abaki la watu hawa ambao wameachiliwa, ikiwa Mungu atawapatia maneno yangu, ili wajue kuhusu vitu vya baba zao; ndiyo, ninawazungumzia, ninyi baki la nyumba ya Israeli; na haya ndiyo maneno ambayo ninasema:

2 Nataka mjue kwamba ninyi ni wa anyumba ya Israeli.

3 Nataka mjue kwamba lazima mtubu, au hamtaokolewa.

4 Nataka mjue kwamba lazima muweke chini silaha za vita, na msifurahie tena katika umwagaji wa damu, na msizichukue tena, isipokuwa kama Mungu atawaamuru.

5 Nataka mjue kwamba lazima amuelimike kuhusu babu zenu, na mtubu dhambi zenu zote na maovu, na bkuamini katika Yesu Kristo, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu, na kwamba aliuawa na Wayahudi, na kwa uwezo wa Baba amefufuka tena, kwa kufanya hivyo amepata cushindi juu ya mauti; na pia kupitia kwake uchungu wa kifo umetolewa.

6 Na anatimiza aufufuo wa wafu, ambako binadamu lazima atainuliwa kusimama mbele ya bkiti cha hukumu.

7 Na ameleta kutimizwa aukombozi wa ulimwengu, ambako yule ambaye atapatikana bila bmakosa mbele yake katika siku ya hukumu atakubaliwa ckuishi kwenye uwepo wa Mungu katika ufalme wake, kuimba sifa zisizo na mwisho na jamii ya dwaimbaji wa juu, kwa Baba, na kwa Mwana, na kwa Roho Mtakatifu, ambao ni eMungu mmoja, katika hali ya ffuraha ambayo haina mwisho.

8 Kwa hivyo tubuni, na mbatizwe katika jina la Yesu, na mkubali ainjili ya Kristo, ambayo itawekwa mbele yenu, sio tu kwa maandishi haya lakini pia kwa bmaandishi ambayo yatawajia Wayunani ckutoka kwa Wayahudi, maandishi ambayo yatatoka kwa Wayunani dhadi kwenu.

9 Kwani tazama, ahaya yameandikwa kwa kusudi kwamba bmngeamini hayo; na mkiyaamini hayo mtaamini haya pia; na ikiwa mtaamini haya mtajua kuhusu babu zenu, na pia kazi za ajabu ambazo zimesababishwa na uwezo wa Mungu miongoni mwao.

10 Na mtajua pia kwamba ninyi ni baki la uzao wa Yakobo; kwa hivyo mmehesabiwa miongoni mwa watu wa agano la kwanza; na ikiwa itakuwa hivyo kwamba mtaamini katika Kristo, na mnabatizwa, kwanza kwa maji, halafu kwa moto na Roho Mtakatifu, mkifuata amfano wa Mwokozi wetu, kulingana na alivyotuamuru, itakuwa vema nanyi katika ile siku ya hukumu. Amina.