Maandiko Matakatifu
2 Nefi 19


Mlango wa 19

Isaya anazungumza kiumasiya—Watu wale walio gizani wataona nuru kuu—Kwetu sisi mtoto amezaliwa—Atakuwa Mwana Mfalme wa Amani na atatawala kwenye kiti cha enzi cha Daudi—Linganisha Isaya 9. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Walakini, giza halitakuwa kubwa kama ilipokuwa katika dhiki yake aliposhambuliwa, wakati hapo mwanzoni alitesa kidogo anchi ya Zabuloni, na nchi ya Naftali, na baadaye kwa uzito akapitia kwa njia ya Bahari ya Shamu ngʼambo ya Yordani katika Galilaya ya mataifa.

2 Watu wale waliotembea agizani wameona nuru kuu; wale wanaoishi katika nchi ya kivuli cha kifo, wameangaziwa na nuru.

3 Umeliongeza taifa, na akuzidisha shangwe—wanajaa shangwe mbele yako kulingana na shangwe ya mavuno, na kama vile watu wanavyofurahia wanapogawana nyara.

4 Kwani umevunja nira ya mzigo wake, na gogo la bega lake, fimbo ya yule anayemdhulumu.

5 Kwani kila vita vya askari shujaa huunganishwa na makelele, na mavazi yaliyovingirishwa kwenye damu; lakini hii itakuwa ni ya kuchomwa na kuwa makaa ya moto.

6 Kwani kwetu sisi amtoto amezaliwa, kwetu tumepewa mwana; na bserikali itakuwa kwenye bega lake; nalo jina lake litaitwa, Ajabu, Mshauri, cMwenyezi Mungu, dBaba asiye na mwisho, Mwana Mfalme wa eAmani.

7 Na ahakuna mwisho wa upanuzi wa bserikali na amani, katika kiti cha enzi cha Daudi, na juu ya utaratibu wa ufalme wake, na kuiimarisha kwa hukumu na kwa haki tangu sasa, na hata milele. Bidii ya Bwana wa Majeshi itatenda haya.

8 Bwana alimtumia Yakobo neno lake na limemulikia aIsraeli.

9 Na watu wote watajua, hata Efraimu na wakazi wa Samaria, wanaosema kwa kiburi na ugumu wa moyo:

10 Matofali yameanguka chini, lakini sisi tutajenga kwa mawe yaliyochongwa; mikuyu imekatwa, lakini sisi tutaibadilisha iwe mierezi.

11 Kwa hivyo Bwana atawainua maadui wa aResini dhidi yake, na kuwaunganisha maadui wake pamoja;

12 Waashuri mbele yao na Wafilisti nyuma yao; na awatamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Lakini hata baada ya haya bhasira yake haitapungua, lakini bado amenyoosha mkono wake.

13 Kwani watu ahawatamrejea aliyewapiga, wala kumtafuta Bwana wa Majeshi.

14 Kwa hivyo Bwana atakata kutoka Israeli kichwa na mkia, tawi na tete katika siku moja.

15 Mzee, ndiye kichwa; na nabii anayefundisha uwongo, ndiye mkia.

16 Kwani viongozi wa watu hawa wanawasabisha wakose; na wale wanaoongozwa nao wanaangamia.

17 Kwa hivyo Bwana ahatakuwa na shangwe katika vijana wao, wala hatawahurumia yatima wao na wajane wao; kwani kila mmoja wao ni mnafiki na mwovu, na kila mdomo unanena bupumbavu. Kwa haya yote hasira yake haitapungua, lakini bado amenyoosha cmkono wake.

18 Kwani uovu huteketea kama moto; itaila mibigili na miiba, na itawasha vichaka vya mwitu, na yatapaa juu kama kuinuka kwa moshi.

19 Kwa kupitia ghadhabu ya Bwana wa Majeshi nchi inatiwa giza, na watu hao watakuwa kama makaa ya moto; ahakuna mtu yeyote atakayemhurumia kaka yake.

20 Na atapokonya upande wa mkono wa kulia na kuwa na njaa; na aatakula kwa upande wa mkono wa kushoto na hawatatosheka; kila mtu atakula nyama ya mkono wake mwenyewe—

21 aManase dhidi ya bEfraimu; na Efraimu dhidi ya Manase; wao wawili pamoja watamshambulia cYuda. Kwa haya yote hasira yake haitapungua, lakini bado amenyoosha mkono wake.