Maandiko Matakatifu
Moroni 4


Mlango wa 4

Namna wazee na makuhani wanavyohudumia sakramenti ya mkate inaelezwa. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 aNjia ya bwazee wao na makuhani wakibariki mwili na damu ya Kristo kwa washiriki; na cwaliubariki kulingana na amri za Kristo; kwa hivyo tunajua njia ni ya kweli; na mzee au kuhani aliibariki—

2 Na walipiga magoti chini na washiriki, na kuomba kwa Baba katika jina la Kristo, wakisema:

3 Ee Mungu, Baba wa Milele, tunakuomba katika jina la Mwanao, Yesu Kristo, ubariki na utakase amkate huu kwa roho za wale wote watakaoula, ili waweze kuula kwa bukumbusho wa mwili wa Mwanao, na wakushuhudie, Ee Mungu, Baba wa Milele, kwamba wako radhi kujichukulia juu yao cjina la Mwanao, na daima kumkumbuka, na kushika amri zake ambazo amewapa, ili daima dRoho wake apate kuwa pamoja nao. Amina.