Maandiko Matakatifu
Mosia 1


Kitabu cha Mosia

Mlango wa 1

Mfalme Benjamini anafundisha wanawe lugha na unabii wa babu zao—Dini yao na utamaduni wao zimehifadhiwa kwa sababu ya maandishi yaliyowekwa kwenye mabamba mbali mbali—Mosia anateuliwa kuwa mfalme na kupewa jukumu la kuhifadhi yale maandishi na vitu vingine. Karibia mwaka 130–124 K.K.

1 Na sasa kulikuwa hakuna ubishi katika anchi yote ya Zarahemla, miongoni mwa watu wote wa mfalme Benjamini, hata kwamba mfalme Benjamini akawa na amani katika siku zake zote zilizo salia.

2 Na ikawa kwamba alipata wana watatu; na akawaita majina yao, Mosia, na Helorumu, na Helamani. Na akasababisha kwamba awafundishwe kwa blugha yote ya babu zake, ili wawe watu wenye ufahamu; na ili wajue kuhusu unabii uliokuwa umezungumzwa kwa vinywa vya babu zao, ambao ulikuwa umetolewa na mkono wa Bwana.

3 Na pia akawafundisha kuhusu kumbukumbu ambazo zilikuwa zimechorwa kwenye yale mabamba ya shaba nyeupe, akisema: Wana wangu, nataka mkumbuke kwamba kama sio amabamba haya, ambayo yana kumbukumbu hizi na amri hizi, lazima tungeteseka kwa bkutojua, mpaka wakati huu, kwa kutojua siri za Mungu.

4 Kwani haingewezekana kwamba baba yetu Lehi, angevikumbuka vitu hivi vyote, kuvifundisha kwa watoto wake, bila usaidizi wa mabamba haya; kwani yeye alikuwa amefundishwa kwa alugha ya Wamisri kwa hivyo yeye aliweza kusoma michoro hii, na kuwafundisha watoto wake, ili nao wawafundishe watoto wao, na hivyo kutimiza amri za Mungu, hadi wakati huu.

5 Nawaambia, wana wangu, kama sio kwa sababu ya vitu hivi, ambavyo vimewekwa na akuhifadhiwa kwa mkono wa Mungu, ili btusome na tufahamu csiri zake, na tuwe na amri zake kila mara machoni mwetu, hata kwamba baba zetu wangefifia katika kutoamini, na tungekuwa kama ndugu zetu, Walamani, ambao hawajui lolote kuhusu vitu hivi, au hata kwamba hawaviamini wanapofundishwa, kwa sababu ya ddesturi za baba zao, ambazo sio sawa.

6 Enyi wana wangu, ningependa mkumbuke kwamba hii misemo ni ya kweli, na pia kwamba maandishi haya ni ya akweli. Na tazama, pia mabamba ya Nefi, ambayo yana maandishi na misemo ya baba zetu tangu walipotoka Yerusalemu hadi sasa, na ni za kweli; na tunaweza kujua ukweli wao kwa sababu ziko mbele machoni mwetu.

7 Na sasa, wana wangu, ningependa kwamba amyapekue kwa bidii, ili mfaidike; na ningependa kwamba bmtii amri za Mungu, ili cmfanikiwe nchini kulingana na dahadi ambazo Bwana aliwafanyia babu zetu.

8 Na ni vitu vingi zaidi ambavyo mfalme Benjamini aliwafundisha wanawe, ambavyo havijaandikwa kwenye kitabu hiki.

9 Na ikawa kwamba baada ya mfalme Benjamini kumaliza kuwafundisha wanawe, kwamba alizeeka, na akaona kwamba lazima hivi karibuni aelekee katika ile njia ya ulimwengu wote; kwa hivyo, akadhani kwamba ni muhimu aukabidhi ufalme wake kwa mmoja wa wanawe.

10 Kwa hivyo, akasababisha Mosia asimamishwe mbele yake; na haya ndiyo maneno ambayo alimzungumzia, akisema: Mwana wangu, nataka utangaze kote nchini hii miongoni mwa watu hawa wote, au awatu wa Zarahemla, na watu wa Mosia ambao wanaishi katika nchi hii, kwamba wakusanyike pamoja; kwani kesho nitawatangazia watu wangu kwa kinywa changu kwamba wewe ni bmfalme na mtawala juu ya hawa watu, ambao Bwana Mungu wetu ametupatia.

11 Na juu ya hayo, nitawapatia watu hawa ajina, ili waweze kutofautishwa kutokana na watu wote ambao Bwana Mungu aliwatoa kutoka nchi ya Yerusalemu; na hivi ninatenda kwa sababu wamekuwa watu wa bidii kwa kutii amri za Bwana.

12 Na ninawapa jina ambalo halitafutwa, ila tu kwa adhambi.

13 Ndiyo, na zaidi ninakwaambia, kwamba ikiwa watu hawa walioheshimiwa na Bwana zaidi wataanguka kwenye adhambi, na wawe waovu na watu wazinifu, kwamba Bwana atawatoa, ili wawe bwanyonge kama ndugu zao; na chatawalinda tena kwa nguvu zake zisizokuwa na kipimo; kama vile alivyowahifadhi babu zetu.

14 Kwani ninakwambia, kwamba kama hangenyosha mkono wake kuwahifadhi babu zetu lazima wangeanguka mikononi mwa Walamani, na waumie kwa sababa ya chuki yao.

15 Na ikawa kwamba baada ya mfalme Benjamini kumaliza kumzungumzia mwana wake, kwamba aliweka mikononi mwake mambo yote ya ufalme.

16 Na zaidi ya hayo, aliweka mikononi mwake kuhusu zile kumbukumbu ambazo ziliyochorwa kwenye amabamba ya shaba nyeupe; na pia mabamba ya Nefi; na pia, bupanga wa Labani, na cmpira au kielekezo, ambacho kiliwaelekeza babu zetu kupita nyikani, ambacho kilitayarishwa na mkono wa Bwana ili waelekezwe, kila mmoja kulingana na utiifu na bidii waliompatia.

17 Kwa hivyo, kwa vile hawakuwa waaminifu hawakufanikiwa wala kuendelea katika safari yao, lakini awalirudishwa nyuma, na kujiteremshia hasira ya Mungu juu yao; na kwa hivyo walipigwa kwa njaa na maumivu makali, ili kuwavuruga wakumbuke jukumu lao.

18 Na sasa, ikawa kwamba Mosia alienda na kutenda kulingana na yale baba yake aliyomwamuru, na kuwatangazia watu wote waliokuwa katika nchi ya Zarahemla kwamba wajikusanye pamoja, ili waende kwenye hekalu kusikiliza maneno ambayo baba yake atawazungumzia.