Muziki
Kwa Nyimbo za Utukufu


32

Kwa Nyimbo za Utukufu

Kwa furaha

1. Kwa nyimbo za utukufu,

Twamwabudu Bwana,

Twampatia shukrani

Kwa kutukomboa.

[Chorus]

Njoo mbele za Mungu!

Mfanye ibada!

Semeni haja za moyo

Hata kwa kuimba.

2. Wimbo wa waadilifu

Ni sala kwa Bwana;

Wamkaribisha Roho,

Watujumuisha.

[Chorus]

Njoo mbele za Mungu!

Mfanye ibada!

Semeni haja za moyo

Hata kwa kuimba.

3. Hapo kale Ibrahimu

Aliimba nyimbo;

Wimbo mpya tutaimba

Akirudi Kristo.

[Chorus]

Njoo mbele za Mungu!

Mfanye ibada!

Semeni haja za moyo

Hata kwa kuimba.

Maandishi: Penelope Moody Allen, kuz. 1939. © 1985 IRI

Muziki: Newel Kay Brown, kuz. 1932. © 1985 IRI

Zaburi 30:4

Mafundisho na Maagano 25:12