76
Sala ya Faragha
Kwa kutafakari
1. Kuna muda mtulivu,
Pasipo karaha;
Mbele ya Bwana nasali
Sala ya faragha.
[Chorus]
Moyo na ugeuke,
Kuomba siku zote,
Na ili nafsi yangu
Iungane na mbingu.
2. Njia nyofu ya mbinguni,
Wapo malaika,
Twaipata tufanyapo,
Sala ya faragha.
[Chorus]
Moyo na ugeuke,
Kuomba siku zote,
Na ili nafsi yangu
Iungane na mbingu.
3. Dhoruba nipitiapo,
Ni faraja kwamba,
Bwana husikia ile,
Sala ya faragha.
[Chorus]
Moyo na ugeuke,
Kuomba siku zote,
Na ili nafsi yangu
Iungane na mbingu.
4. Adui anitegapo,
Mwokozi namwita,
Huja kama nitasali,
Sala ya faragha.
[Chorus]
Moyo na ugeuke,
Kuomba siku zote,
Na ili nafsi yangu
Iungane na mbingu.
Maandishi na muziki: Hans Henry Petersen, 1835–1909
Mathayo 6:6