Muziki
Nitamfuata


192

Nitamfuata

Kwa ujasiri

1. Bwana amenipa injili.

Nimefunzwa tangu utotoni.

Nitashiriki nuru ya haki

Kumshuhudia.

Bwana amenipa imani.

Atanijibu nitaposali.

Nitatumika na kwa furaha

Nitamfuata.

2. Bwana amenipa upendo.

Nimefunzwa kupitia Roho.

Hivyo nitakuwa mwaminifu

Kwa kuwa mkweli.

Nimebarikiwa na Yesu,

Kwa shukurani nitamsifu,

Nimeamua, kumtangaza.

Nitamfuata.

Nitathamini njia ya kweli,

Nitamfuata.

Maandishi na muziki: Janice Kapp Perry, kuz. 1938

© 2001 na Janice Kapp Perry. Haki zote zimehifadhiwa. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.