Muziki
Tuliishi kwa Baba


179

Tuliishi kwa Baba

Kwa urahisi

1. Kweli hapo kale tuliishi kwa Baba

Tukipendwa na watu tuliowajua.

Ndipo Mungu akaleta mpango wake

Wa wokovu na wa maisha ya milele.

2. Baba alitaka mwenye pendo la kweli

Wa kutukomboa ili kwake turudi.

Mwingine alitaka heshima tukufu.

Yesu alisema, “Utukufu kwa Mungu.”

3. Yesu akatumwa kuja kama Masiya;

Kwa jina lake Ibilisi akashindwa.

Anatupa matumaini ya kuishi

Mbinguni kwa Baba anakotusubiri.

Maandishi na Muziki: Janeen Jacobs Brady, kuz. 1934

© 1987 na Janeen Jacobs Brady. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.