Muziki
Ninakuhitaji


47

Ninakuhitaji

Kwa hamasa

1. Ninakuhitaji,

Ewe Bwana.

Hakuna mwingine

Kuniponya.

[Chorus]

Yesu nakuhitaji;

Muda wote Bwana!

Nibariki Mwokozi;

Naja kwako!

2. Ninakuhitaji;

Kwangu njoo.

Jaribu hushindwa

Ukiwepo.

[Chorus]

Yesu nakuhitaji;

Muda wote Bwana!

Nibariki Mwokozi;

Naja kwako!

3. Ninakuhitaji,

Muda wote.

Njoo kwa haraka,

Niwezeshe.

[Chorus]

Yesu nakuhitaji;

Muda wote Bwana!

Nibariki Mwokozi;

Naja kwako!

4. Ninakuhitaji,

Bwana Mungu.

Nifanye wa kwako,

Mtukufu!

[Chorus]

Yesu nakuhitaji;

Muda wote Bwana!

Nibariki Mwokozi;

Naja kwako!

Maandishi: Annie S. Hawks, 1835–1918

Muziki: Robert Lowry, 1826–1899

2 Nefi 4:16–35

Zaburi 143:1