71
Amri Zake Mungu
Kwa utulivu
1. Amri zake Mungu
Ni njema hakika!
Mtwike mzigo wako,
Na atakutunza.
2. Kwenye lindo lake,
Wema huwalea.
Mkono wake mkuu
Wana huwalinda.
3. Mzigo wa hofu,
Usikuangushe.
Kimbilia kwake Baba
Nguvu upatiwe.
4. Wema wake kwetu
Haubadiliki;
Nitautua mzigo,
Na nitafurahi.
Maandishi: Philip Doddridge, 1702–1751
Muziki: Hans Georg Nägeli, 1773–1836; umepangiliwa na Lowell Mason, 1792–1872
1 Yohana 5:3
Zaburi 55:22