Muziki
Shangwe Kote


113

Shangwe Kote

Kwa shangwe

1. Shangwe kote, Bwana aja;

Mfalme, karibu!

Kila moyo, tayarisha,

Na Watakatifu,

Na Watakatifu,

Nanyi malaika sifu.

2. Yesu atapotawala

Na Wema waimbe,

Mbuga, mito, na vilima

Kote warudie,

Kote warudie,

Zao shangwe na zivume.

3. Majonzi yatakomeshwa,

Pia na mateso;

Atakuja kuzifanya

Baraka ziwemo,

Baraka ziwemo,

Kote laana ilipo.

4. Shangwe! Kwa Aliye Juu,

Sayuni yakua

Kama nyota kwenye mbingu,

Milele daima,

Milele daima

Mungu zinamtukuza.

Maandishi: Isaac Watts, 1674–1748; Yamebadilishwa na William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.

Muziki: George F. Handel, 1685–1759; Umepangiliwa na Lowell Mason, 1792–1872

Alma 5:50

Zaburi 97:1

Zaburi 98:4–9