Muziki
Asubuhi Ile Njema


15

Asubuhi Ile Njema

Kwa heshima

1. Asubuhi ile njema!

Jua likachomoza.

Na sauti zao ndege,

Zote zilisikika.

Hapo katika kisitu

Joseph kamwomba Baba,

Hapo katika kisitu

Joseph kamwomba Baba.

2. Alipopiga magoti—

Sala yake ya kwanza—

Nguvu za Shetani nazo

Zikamshambulia;

Hakusita kuamini

Mungu atamlinda,

Hakusita kuamini

Mungu atamlinda.

3. Ghafla mwanga ukashuka

Unaozidi jua,

Na mwale wa utukufu

Ukammulikia,

Ndipo wakaja wawili,

Mungu Baba na Mwana,

Ndipo wakaja wawili,

Mungu Baba na Mwana.

4. “Huyu, Mwanangu Mpendwa;

Utamsikiliza!”

Kajibiwa sala yake,

Akamtii Bwana.

Ni furaha iliyoje,

Kumwona Mungu Baba,

Ni furaha iliyoje,

Kumwona Mungu Baba.

Maandishi: George Manwaring, 1854–1889

Muziki: Sylvanus Billings Pond, 1792–1871; umefanyiwa marekebisho na A. C. Smyth, 1840–1909

Joseph Smith—Historia ya 1:14–20, 25

Yakobo 1:5